MIAKA 19 YA NYERERE

Joined
Mar 3, 2018
Posts
75
Reaction score
800
NYERERE ALIJIUZULU MARA 3 KWA MASLAHI YA TANU NA TAIFA ZIMA.

Katika kuadhimisha miaka 19 ya kifo cha Baba wa Taifa nimeona niwashirikishe huu upekee wa NYERERE;

Baada Ya Kuanzishwa Kwa TANU mwaka 1954,wana TANU walimchagua Mwalimu Nyerere Kuwa Rais Wa Chama Chao.

Wakati Huo Yeye alikua ni mwalimu katika shule ya sekondari ya Pugu iliyokua ikiendeshwa na kanisa la RC.

1. MWL NYERERE AJIUZULU UALIMU.

Ili Kanisa La Romani Katholiki lisieleweke vibaya kwa serikali ya wakati huo,walimwomba Nyerere achague kuendelea na ualimu au kuongoza chama cha siasa,kwa hekima yake aliamua kuacha kazi ya ualimu 1955 ambayo ilikua inamlipa sh 500 kwa mwezi ili apate fulsa ya kuongoza TANU kupigania uhuru wa Tanganyika kwa ahadi ya kulipwa sh 500 na chama.

2. NYERERE AJIUZULU UJUMBE WA LEGCO.

Julai 1957,Gavana Sir Edward Twining wa serikali ya kiingereza alimteua mwalimu Nyerere kuwa mjumbe wa baraza la kutunga sheria( Legislative Council Au LEGCO)

Lengo kuu ilikua kumhonga marupurupu ili apunguze domo la kudai uhuru lakini akaamua kujiuzulu tar 14/12/1957 ili asipoteze lengo.

3.Tar 22/01/1962 NYERERE AJIUZULU UWAZIRI MKUU.

Baada Ya Tanganyika Kujitawala Tarehe 09/12/1961, Mwl Nyerere Aliendelea Kama Waziri Mkuu Kwa Siku 44 tu.

Tar 22/01/1962, alijiuzulu uwaziri mkuu na kumchagua mzee RASHID MFAUME KAWAWA kuwa waziri mkuu badala yake na yeye alikua radhi kuendelea kuwa mbunge wa kawaida ili apate nafasi ya kuimarisha TANU ambayo yeye alikua rais wake kwa lengo la kuwafikia watu kupitia chama imara,

Ninanukuu maneno yake;

" leo nimeachia nafasi ya uwaziri mkuu wa tanganyika.
Kabla ya kufanya hivyo mimi mwenyewe nimechagua timu mpya ya mawaziri chini ya uongozi wa bwana Rashidi Kawawa.

(....) Nimechukua Hatua hii na nimeungwa mkono na wenzangu baada ya majadiliano marefu,kwasababu tunaamini kwamba hii ndiyo njia nzuri ya kuyafikia malengo yetu mapya ya kujenga nchi ambamo wananchi watashiriki kwa karibu na kwa ukamilifu katika kupambana na UMASKINI,UJINGA NA MARADHI..."

Viongozi wa sasa hivi ni wa ajabu sana, wanakufa wananchi 229 ( kijiji kizima) lakini wanaendelea kuwa ofisini,wanatekwa watu,wengine wanamiminiwa risasi,wananunua watu ili waupotoshe UMMA halafu hawataki kuwajibika juu ya makosa yao.

Wanataka tuwafananishe na Mwalimu NYERERE tu.

Ifike wakati tusimfananishe Mwalimu Nyerere na mambo ya Kijinga. Ni vizuri kujua kuwa Nyerere alikua mmoja na tulishamzika,hawa wengine watapita tu.

Kitu pekee wanachoweza kufanya watimize wajibu wao,wasishabikie umwagaji damu na utekaji wa watu wanaouratibu wenyewe ili waendelee kuwa watawala. Wakumbusheni kama watapita.

Ni matumaini yangu utakua umejifunza kitu ewe mtanzania!

Chanzo: Maadili Ya Taifa Na Hatma Ya Tanzania,enzi Za Mwalimu, I.M. KADUMA.

Elia F Michael.
Diwani Gwarama.
Mwenyekiti wa Madiwani Kanda ya Magharibi.
Mbunge nje ya Bunge.
Mwalimu Nje ya Darasa.
14/Oktoba/2018.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…