ndandawamalenja
JF-Expert Member
- Nov 1, 2012
- 548
- 656
Miaka 15 hivi iliyopita jamaa yangu wa karibu aliamua kuoa demu ambaye walikuwa wamekutana miezi kama 3 tu iliyopita. Ndani ya kipindi hicho cha miezi mitatu ya kudeti, jamaa akagundua kuwa huyo mke mtarajiwa ana mawasiliano na wanaume wengine wawili. Alipohoji demu akamwambia ni maex wake bado wanamsumbua.
Jamaa akafuatilia akajua ni uongo bado mmoja wao anakula. Kiukweli demu alikuwa mambo mengi na mjanja mjanja sana. Jamaa akaamua kumuoa hivo hivo akiamini demu atatulia. Mara baada ya ndoa tu, jamaa akapata kazi serikalini Ifakara.
Kabla ya hapo alikuwa anafanya na kampuni binafsi hapa hapa Dar. Alipomwambia mkewe (ambaye hata miezi 6 kwenye ndoa hawajatimiza), mwanamke akasema yeye hawezi kuishi nje ya Dar. Akasema yeye njia ya Morogoro mwisho Kibaha, hawezi toka nje ya hapo. Njia ya Bagamoyo mwisho Bunju, uelekeo wa barabara ya Nyerere, mwisho Gongolamboto, na barabara ya Kilwa mwisho ni Mbagara. Hatoki nje ya hapo kimaisha.
Jamaa akaenda Ifakara peke yake. Baada ya miaka 3, upweke ukamshinda akapata demu wa kumpoza akizidiwa. Siku moja mkewe akamtembelea jamaa Ifakara na majirani wakampa umbea kuwa kuna demu anakujaga sana hapo. Alipomuuliza mumewe, mshikaji akamuuliza ikiwa ni kweli atashangaaje wakati anaishi bila mke mwaka wa 3? Basi mwanamke akawa mpole. Akasema anahamia Moro mjini ili jamaa awe anakuja Moro kila ijumaa jioni anaondoka jumapili jioni kurudi kazini Ifakara. Wakakubaliana hivo, mwanamke akahamia Moro mjini. Demu akafungua na biashara za saluni na steshenari. (Ni mpambanaji sana demu).
Maisha yakasonga mpaka wakajenga nyumba Morogoro mjini wakahamia. Wakazaa mtoto wa kwanza, wakaongeza wa pili. Jamaa akamnunulia gari wife ili asipate shida kwenye mizunguko na watoto. Kama kwenda clinic na kadhalika.
Picha likaanza huyu mtoto wa pili alipokuwa na miezi 5. Siku moja jamaa anatoka zake Ifakara anakuja mjini Moro (Bila kumtaarifu mkewe na ilikuwa Alhamisi sio Ijumaa), gari ya mkewe ikawapita mitaa ya njia panda ya Mzumbe, nayo inaelekea mjini. Jamaa akamuona anayeendesha sio mwanamke ni mwanaume. Ila kushoto kakaa mwanamke hakumuona vizuri. Akampigia simu mkewe yuko wapi, mkewe akasema yupo nyumbani amepumzika, kichwa kinamuuna.
Jamaa akauliza hajatoka kabisa siku hiyo? Mwanamke akasema hajatoka kabisa. Basi jamaa akamuomba huyo mshikaji aliyempa lift toka Ifakara kuja Moro waifuatilie hiyo gari. Wakaifuata mpaka Moro mjini ikasimama kwenye kijiwe cha bodaboda. Nao wakasimama nyuma yake kwa mbali kidogo. Jamaa akapigwa na butwaa alivoona mkewe anashuka upande wa abiria anazunguka upande wa dereva halafu jamaa aliyekuwa anaendesha kashuka (Sharobaro flani ana Rasta kati ya kichwa pembeni kanyoa punk, yaani badboy flani hivi).
Wakaagana kwa kiss matata halafu Rasta akaingia kichochoro flani hapo hapo. Mke wa jamaa akawasha gari akaenda zake nyumbani. Jamaa nae akachukua boda akaenda home kwake. Alipogonga mlango dada wa kazi akaja kufungua jamaa akaingia ndani, mpaka chumbani. Akamkuta wife amelala kwa kuzuga huku anabembeleza mtoto. Jamaa akamuuliza tena kama alitoka hata kwenda kufuata dawa, mwanamke akakataa kabisa, kwamba hata chumbani hajatoka siku hiyo.
Basi mshikaji akaamua kufanya uchunguzi. Asubuhi na mapema akarudi kile kituo cha bodaboda aliposhukia yule jamaa. Akamuuliza boda mmoja kuwa anamtafuta jamaa mmoja ana rasta hivi jana alikuja na Subaru nyeusi hapo. Yule boda akageuka kwa bodaboda mwenzie akamwambia "bro hapa anamuulizia bwana ake Jesca". Huyo Jesca ndio mke wa mshikaji sasa. Kumbe maeneo hayo mke wake anakuja sana na anajulikana sana kama demu wa ras, toka kabla mkewe hajapata mimba hata ya mtoto wa kwanza. Jamaa mwenye mke kidogo azimie. Bahati nzuri hata huyo ras mwenyewe alikuwa katoka. Hajui ingekuwaje kama angemkuta.
Basi jamaa akarudi home kinyonge sana. Akakuta wife anatoka eti anaenda clinic na mtoto. Jamaa hakuchoka, akachukua boda akamfuatilia mpaka mkewe akaingia kwenye cafe moja mitaa ile ile karibu kidogo na kwa Ras kama kilometa moja hivi. Hapo jamaa akashuka nae akaenda humo cafe. Sasa ndio akamkuta wife wake na Ras, halafu Ras ndio amepakata katoto kanalia. Jamaa anasema alipowaangalia tu pale pale ndio akajua yule mtoto ni wa Rasta na hata yule mkubwa naye atakuwa wa Rasta (Umri kama miaka 3 hivi). Mkewe jasho likawa linamtoka, akajua mumewe labda anajua kila kitu toka siku nyingi. Jamaa akawasalimu huku anatafakari afanye nini, akashindwa kupata jibu. Akawaaga bila kuongeza neno akarudi nyumbani akiwa frustrated kabisa.
Dakika 10 hazikupita gari ya mkewe ikaingia. Mwanamke akaingia ndani akamkuta jamaa chumbani akaanza kulia. Anaomba msamaha. Jamaa hakujibu kitu akachukua kibegi chake akaenda stendi kutafuta usafiri wa Ifakara, akasepa zake. Aliona akikaa anaweza kuua.
Baada ya siku 5 akaomba ruhusa kazini arudi Moro akajadili na mke wake kuhusu kilichotokea. Akakuta mkewe amebeba kila anachokitaka karudi Dar kwa wazazi wake, na gari kasepa nayo. Jamaa akarudi zake Ifakara akaendelea maisha lengo likiwa ni kusaka uhamisho aende mbali kabisa na ukanda wa Pwani, mfano Ukerewe huko au Mpanda. Bahati mbaya uhamisho ukawa shida miezi 6 ikaisha akiwa Ifakara.
Baada ya miezi 6 ya ukimya mwingi siku moja jioni Jecsa (mkewe) akampigia simu mmewe. Na siku hiyo mshikaji alikuwa kaja kwangu ndio ananisimulia utata uliotokea kwenye ndoa yake miezi 6 nyuma. Jesca anaomba ruhusa auze gari ili apate mtaji afungue saluni apate na hela ya kujikimu. Jamaa akamjibu hiyo gari alimnunulia yeye (mke) hata kuisajili alisajili kwa jina lake (mkewe). Kwa hiyo ni lake kwa asilimia zote alifanyie anachotaka. Hayo maongezi na mimi nasikia. Basi mwanamke akasema asante akakata simu. Wakati huo wooote nyumba yao ya Morogoro Iko wazi anakaa kijana tu anayelinda. Mwanamke yuko Dar kwa wazazi wake kipindi chote hicho.
Baada ya mwaka mmoja jamaa alifanikiwa kuhamishiwa kikazi Tabora. Na ameishi huko miaka 3 tayari akiwa amemove on na anafikiri mwanamke naye ameendelea na maisha yake. Sasa kitu cha ajabu juzi kati hapa mwanamke kapiga simu kwa jamaa eti anaomba kurudi nyumbani. Anaomba na msamaha sana eti wayamalize, waendelee na maisha kama zamani. Jamaa akamuuliza kwani nani alimfukuza hapo nyumbani mpaka anaomba kurudiiiii? Mwanamke yuko kimya tu. Akakata simu.
Sasa jamaa yuko kwenye dilemma na bado ana hasira. Anasema ana wasiwasi atamchinja huyo mwanamke siku akirudi pale kwake morogoro. Yani mkeo azae watoto wawili nje ya ndoa, halafu akimbilie kwao miaka karibu mitano! Sasa hivi anataka kurudi?
Wanajiamini nini hawa viumbe??????