Lububi
JF-Expert Member
- May 3, 2013
- 2,128
- 3,759
Binafs ni mpenzi wa timu ya Simba kitaifa. Lakin inapotokea Kagera sugar( timu ya nyumban) inacheza na timu yoyote sipendi ifungwe na hasa ikiwa Kaitaba! Na hata Yanga( ambayo kwa mechi za ndan sijawai kuitakia ushindi wa ndan) au timu nyingine ya Tanzania inapokuwa na mechi za nje ya nchi napenda ishinde. Mtaalam wa masula ya kijamii aniambie ninasumbuliwa na ukabila au unazi hafifu au ndo uzalendo? Hata leo sikufurahishwa na wana bukoba wengi kuvalia Simba kama vile Kagera sugar sio timu yetu pekee inayotuwakilisha wanakagera.