KITUO cha Afya cha Mwamgongo kilichopo Kigoma Vijijini, kaskazini mwa Ziwa Tanganyika kimepatiwa umeme wa nguvu ya kujua ili kunusuru mazingira hatarishi yaliyopo katika kituo hicho.
Kituo hicho ambacho kina wodi ya kujifungulia kina mama wajawazito, maabara na jokofu la kuhifadhia dawa hakijawahi kupata umeme tangu kilipoanzishwa miaka 14 iliyopita na hivyo kusababisha matatizo makubwa kwa wagonjwa.
Hata hivyo, matatizo hayo hivi sasa yameondoka baada ya Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhonga Said Ruhwanya, kutoa msaada wa vifaa vya umeme wa jua vyenye thamani ya sh milioni 27.
Akikabidhi misaada hiyo, Mhonga alisema alifikia uamuzi huo, baada ya kuguswa na yanayowakabili kina mama. Msaada huo utasaidia vijiji saba ambavyo ni Bugamba, Kagunga, Zashe, Kiziba, Mwamgongo, Mtanga na Kigalye.