Hakikwanza
JF-Expert Member
- Dec 11, 2010
- 4,034
- 1,003
Mheshimiwa Rais pole na kazi za ujenzi wa Taifa letu na majukumu yako ya kila siku. Mheshimiwa Rais toka uchaguliwe na kuapishwa mimi binafsi na jamii inayonizunguka tuliamini kuwa sasa tumempata kiongozi wa nchi atakaye iongoza nchi katika misingi ya haki,usawa na utawala bora.
Rais wangu ulianza vyema mwanzoni mwa awamu hii lakini naona tunakoendelea unapoteza dira ulioanzanayo na kutuacha wananchi tukiwa na maswali mengi yasiyopata majibu.
Mheshimiwa Rais hotuba zako nyingi zimekuwa za kuvunja matumaini ya wananchi wanyonge kutokana na kauli zenye kukatisha tamaa na kuonyesha umemeza madaraka yote.Mfano kauli yako ya kuwa unajua wewe mwenyewe nani anatakiwa kuwa wapi akae wapi ni wewe unayepanga, hii kauli ukiifatilia kwa kina inamaana maamuzi hayafanyiki na Rais kama taasisi bali Rais kama wewe binafsi nacho kifahamu kiongozi lazima ashirikishe vyombo alivyonavyo ndani ya taasisi anayoiongoza ilikufikia maamuzi yaliyosahihi. Nikisikiliza kauli hiyo napata shida kama kunakupokea ushauri toka kwa washauri wako.
Mheshimiwa Rais kauli hiyo umeitoa ukiwa katika harakati za kumlinda mkuu wa mkoa wa DSM Mheshimiwa Paul Makonda; Ni kweli naye alianza vizuri katika hiyo nafasi lakini huku alikofika unatakiwa umpatie nafasi ya kupumzika kwani anachokifanya sasa ni shida tupu na anakiuka misingi ya uongozi bora. Mheshimiwa Rais kiongozi bora ni yule anayepima jema na baya na kuamua kuchukua jema na kulifanyia kazi kwa manufaa ya watu anao waongoza lakini hiki kinachoendelea ni kizungumkuti.
Mheshimiwa Rais angalia ulikotoka umepita mabonde na milima mingi sana hivyo kaa ukijua Watanzania tuna matarajio makubwa kutoka katika taasisi yako kwani ndio usukani wa nchi vinginevyo tutaanguka kabla ya kufika. Pia ni vema hotuba zako zikawa za kuleta umoja wa kitaifa na sio kuligawa taifa kama iliyohusu wabunge wa CCM kuwapa muda wapinzani na kuwakemea wabunge waliokuwa wanataka kwenda kumwona Mh Lema. Ingawa wewe ni Mwenyekiti wa CCM pia ni Rais wa nchi hivyo umakini wa maamuzi ni muhimu. Wewe ni baba wataifa epuka kubagua wote ni wako, upinzani na wasio upinzani, wenye dini na wasio na dini, wasafi na wachafu, wakulima na wafugaji, wenye akili na wasio na akili, wazima na wagonjwa.
Mwisho nakuomba uliunganishe taifa tuwe kitu kimoja tuepuke roho za visasi, uadui na husuda. Hapo tutajenga taifa moja lenye nguvu na kuheshimiana. Msemakweli ni mpenzi wa Mungu