Mheshimiwa Rais Magufuli: Irejeshe Mbeya Medical Research Center kwa Wajerumani

JembeNaNyundo

JF-Expert Member
Dec 9, 2016
533
652
Nilishawahi fanya internship pale Mbeya Referral Hospital, ambayo sasa wanaiita Southern Highlands Zonal Referral Hospital au Mbeya Zonal Referral Hospital. Hii ni hospitali ya pili kubwa ya Serikali, baada ya Muhimbili National Hospital (sahau Bugando, na hata KCMC maana si hospitali za serikali).

Ndani ya Mbeya Referral Hospital kuna taasisi ambayo enzi hizo ilikuwa ikiitwa Mbeya Medical Research Programme (MMRP). MMRP ilianzishwa kwa ushirikiano wa Chuo Kikuu cha Munich, ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na Mbeya Referral Hospital. Baadaye University of Munich wakatafuta pesa na kuijenga MMRP kwa kusimamisha majengo kadhaa likiwemo jengo la ghorofa mbili na pia wakaki equip na vifaa vya kisasa vya maabara. Kwa sehemu wakawa wakiisaidia pia hiyo Mbeya Referral Hospital.

MMRP ilikuwa ni taasisi iliyokuwa ikiongozwa na Prof. Michael Hoelscher, wa chuo kikuu cha Munich. Prof. Hoelscher alisifika kwa kuingiza miradi mikubwa mikubwa ya utafiti ambayo ilileta sifa za kitafiti na ajira nyingi sana. Moja ya utafiti kubwa alizoleta ni kama ule uliokuwa ukiitwa RV172, ambao ulikuwa ni utafiti wa chanjo ya UKIMWI wa kwanza nchini Tanzania (achana na ule wa Muhimbili uliokuja baadaye sana, ambao kiuhalisia walijifunzia kwa hawa MMRP). Pia kulikuwa na tafiti kama EMINI n.k. Kituo hiki kilijenga sifa kwa Taifa, na pia kiliwasaidia watanzania wengine kujiendeleza kielimu hadi kiwango cha PhD.

Kulikuwa na figisu figisu nyingi sana za kuwanyang'a hawa wajerumani hiki kituo, na moja ya sababu ilikuwa tamaa ya madaraka, ulafi na hamu ya taasisi ya taifa ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) kuhodhi vituo vingi chini yake ingawa hawana pesa za kuviendesha. Miaka miwili mitatu iliyopita, hiki kituo kilichukuliwa na NIMR baada ya kushinda figisufigisu kibao, na kisha kubadirishwa jina kuitwa NIMR - Mbeya Medical Research Center au NIMR-MMRC. MMRP na baadaye NIMR-MMRC ndipo Mkurugenzi wa sasa wa TACAIDS Dr. Maboko alikuwa akifanya kazi kama Mkurugenzi wa kituo. Alikuwa kama msaidizi wa Prof. Michael Hoelscher.

Baada ya kuchukuliwa kwa kituo hiki, upatikanaji wa pesa za miradi umekuwa ni shida kubwa. Hali ya kifedha ya kituo imekuwa mbaya sana. Na pia ile miradi mikubwa ya UTAFITI imepotea. Wajerumani waliponyang'anywa kituo waliamua kuhama Tanzania na kwenda Msumbiji ambako wameanzisha kituo kipya kabisa, na serikali ya huko imewapa majengo na ardhi kubwa wafanye mambo ya utafiti kwa amani.

Mheshimiwa Rais, hawa wazungu walifanyiwa ndivyo sivyo kwa kunyang'anywa kituo hiki. Mimi ningekushauri warejeshewe kituo chao. Na wale watumishi waliohamishiwa NIMR, waendelee kuwa watumishi wa NIMR lakini wapate ujuvi kupitia hawa wazungu, ambao kweli wako mbali katika nyanja za utafiti na pia kuzitafuta pesa za miradi.

Kituo cha MMRP kilikuwa kinainuka kwa kasi kubwa, kiasi kwamba ilibaki kidogo tu kiifikie IFAKARA HEALTH INSTITUTE ambayo nayo kukua kwake kumekuwa rahisi saana baada ya kutoingiliwa na serikali.

Tumtafute Prof. Michael Hoelscher aje aendeleze kituo chake kwa ushirikiano na watanzania. Tunapata faida nyingi zaidi akiwepo, kuliko tulipomfukuza. Hata ukienda pale NIMR-MMRC kamuulize hadi mfagiaji kama atapenda Mjerumani arudi watakwambia NDIO.
 
Mkuu hayo ndio matokeo ya kuchanganya siasa na taaluma. Hata hapo unapoomba msaada...sijui! Labda amalizane kwanza na mchanga.
 
Back
Top Bottom