Mheshimiwa Mwigulu Mchemba aache kupotosha wa-Tanzania.

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,205
2,690
Mheshimiwa Mwigulu Mchemba aache kupotosha wa-Tanzania.

Kuna mahali nimeona Naibu waziri wa fedha –sera akijinasibu eti CCM wagombea wake zaidi ya nusu wamepita bila kupingwa Tanzania nzima, huu ni upotoshaji wa hali ya juu kwa upande wa waziri tena inaonyesha yeye ni mbumbu kwa upande wa masuala ya fore casting.
Nina sababu kadhaa za kithibitisha uwongo wake.

1. Majina ya wagombea yamebandikwa jana saa 10 yeye takwimu hizo kazipata wapi ukitilia maanani Tanzania ni kubwa.

2. Kuna pia zoezi la kuweka pingamizi halijafanyika bado Mwigulu amejihakikishiaje kwamba Mapingamizi yote CCM itashinda

3. Mimi niko Mtwara kata ya Kiromba juu, kwa mjibu wa makubaliano ya UKAWA hapa ni eneo la CUF, Vijiji vyote Kiromba juu yenyewe, Mkahala, Mpanyani na Kianga vijiji vyote, vitongoji vyote kuna wapinzani mbaya kuliko zote kuna kitongoji Fulani mgombea wa CCM kaingia mitini wa CUF kapita bila kupingwa, waziri kapata wapi takwimu hizo aache upuuzi wake.

4. Labda walikoshinda ni kwenye jimbo lake la Iramba ambako majitu bado hayajitambui.

Hivi naibu waziri ni mpumafu nini CCM ipite bila kupingwa wakati watu tuna hasira ya wizi wao huo account ya ASCROW Tegeta, wapite bila kupingwa kwa lipi?
 
Mwigulu ndo shetani, hela zinaibwa yeye yupo kukenua kama nyani. Mkoa wa kagera ukb watashinda kwa 80%
 
Amesahau na kule Geita ambako mgombea wa CCM amewekewa pingaizi kwa kudanganya umri eti kazaliwa tarehe 02.10.2014
 
Back
Top Bottom