GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Nakumbuka kabisa kuna Sheria ilipitishwa ya udhibiti wa makelele hasa ya upigwaji wa mziki kwa sauti kubwa au wahubiri fulani wa Makanisani kutupigia kelele kwa Mahubiri yao au nyimbo zao usiku kucha.
Kinachonisikitisha hili jambo tulitangaziwa na hadi kuaminishwa kuwa litakuwa na utekelezaji madhubuti na litadhibitiwa lakini hadi hivi sasa " natiririka " hivi hali ni ile ile ya Makelele kwa mtindo mmoja na tena nadhani sasa baada ya Mamlaka husika kuzuia hali ndiyo imezidi na huku mitaani hakukaliki.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar Comrade Paul Makonda hili jambo LINAKERA na LINAUDHI mno kwani sasa Mtu ukiamka unaamshwa na kelele na ukirudi kutoka Ofisini unakuta kelele achilia mbali zile kelele za Bosi Ofisini yaani ni " vulu vulu " tu.
Kuna tafiti kama mbili tatu zilifanyika hapa Dar mwaka huu huu na kusema kuwa 75% ya Wakazi wa Dar ni WENDAWAZIMU tofauti ni VIWANGO vyetu tu na inawezekana wengi wetu huu UWENDAWAZIMU wetu UNAHISANIWA kwa kiasi kikubwa na UDHAMINI wa Kero hii kubwa ya kupigizana makelele siku nzima huku mitaani kwetu.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kwakuwa inaonekana upo busy sana na Majukumu ya Madawati na Matamasha unaonaje ukituruhusu tu sisi Raia TUJICHUKULIE tu SHERIA mkononi ili huku huku mitaani TUADHIBIANE wenyewe kimya kimya hadi kitakapoeleweka na Wewe tutakuletea tu mrejesho wa idadi ya Watu tuliyowavunja TAYA, MENO, Kuwatoa NUNDU na kuwavimbisha UGOKO halafu utatusaidia tu kuwatibu katika Hospitali zako za Amana, Mwananyamala na Temeke.
Halafu tunakuomba pia katika hizi hizi Sheria muongeze kipengele cha WAPANGAJI wa nyumba nao kutopigiana kelele kwani hili nalo ni tatizo kubwa hasa kwa sisi TULIOPANGA. Kwa mfano asubuhi ya leo tu tena Saa 11 jirani yangu tu hapa ambaye dirisha lake na langu lipo karibu kaamka zake tu huo muda kaanza kupiga miziki ya " Singeli " na kama haitoshi kaongeza sauti ya juu kabisa na cha kuudhi kabisa wakati ameongeza hiyo sauti kubwa ya mziki yeye katoka ndani mwake na kwenda sehemu ya mbali kabisa kukaa huku akiongea na Simu akiwa ameridhika kabisa.
Nimeamua kuanza na Wewe Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kabla ya kwenda kwa NEMC ambao nawafananisha na Joka kubwa lakini lisilo na meno na lipo lipo likiwa la " hovyo hovyo ".
Naomba kuwasilisha na nitashukuru ukinijibu Mkuu na sana sana ukitupa go ahead sisi TULIOCHOKA na huu UPUUZI tuweze KUADABISHANA wenyewe kwa wenyewe.