Kwa wanaofuatilia siasa za nchi hii wanaifahamu vizuri Pemba! Kama kuna eneo ambalo Tanzania hii wanaweza kupita kifua mbele kwamba wameikataa CCM hapa duniani hadi akhera, basi eneo hilo si Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mbeya wala Dar es salaam bali ni Pemba!
Mwaka jana endapo Lowassa angesimama kwa tiketi ya CCM basi CCM wangepata kura nyingi sana huko Arusha! Endapo Mark Mwandosya angesimama kwa tiketi ya CCM; basi CCM ingezoa kura nyingi sana huko Mbeya! Kanda ya Ziwa ilionekana tayari wameshaikataa CCM lakini ile kusimamishiwa Msukuma mwenzao tu; harakati za kuikataa CCM wakazipeleka likizo!
Huku bara CCM haijakataliwa kivile bali tuna ushabiki kwa ajili ya watu wetu kwa kuangalia tutokako (regional location), makabila yetu, dini zetu na upumbavu mwingine kama huo!
Ningependa kuwakumbusha wafanya maamuzi wa nchi hii kwamba siasa za Pemba ni tofauti kabisa na bara. Pemba hawajali ikiwa aliyesimama ni mtu wa Unguja au wa Pemba; so long as ni wa CCM watamkataa tu ima fahima! Salim Ahmed Salim yule na umaarufu wake wote ule; ingawaje ni Mpemba lakini akisimama kwa tiketi ya CCM atapewa za uso kama ambavyo alipewa Dr. Shein!
Wapemba wana msimamo pengine kuliko jamii nyingine yoyote ile nchi hii! Hata wakati mahali kama Arusha na Kilimanjato ikiwa dominated na CCM; Mpemba enzi hizo hakuona taabu kusafiri toka Dodoma hadi Pemba kwa ajili tu ya kwenda kupiga kura in favor of CUF!
Kama nilivyogusia hapo juu, lengo la utangulizi huu ni kuwakumbusha wafanya maamuzi-- wasione ukimya na utulivu uliopo hivi sasa Zanzibar halafu wakajidanganya wamewa-contain! Kilichopo hivi sasa huko Zanzibar sio utulivu bali wafuasi wa CUF kusubiria updates kutoka kwa viongozi wao za nini wafanye. Wakiambiwa waingie kwenye uchaguzi tena watakubali bila tatizo na wakiambiwa kinyume chake, watafanya kwa moyo ule ule-- darasa hapa liwe sakata la KURA ZA MARUHANI na Januari 26, 2001.
Kama ilivyo ada, Uchaguzi Mkuu ambao ulifanyika Oktoba 29, 2000 ulivurugwa huko Zanzibar. Sina haja ya kurejea kwa undani dosari za uchaguzi huo lakini itoshe tu kusema kwamba, baada ya kuvurugika kwa uchaguzi, sawa na uchaguzi wa 2015, CCM wakataka kurudiwa kwa uchaguzi lakini CUF wakakataa!
Januari 27, 2001 CUF waliitisha maandamano kwa kile ambacho wenyewe walikiita “chama kingeshirikiana na watu kudai haki yao kwa njia yoyote watakayo amua….!”
Kila mmoja anafahamu, wito ule wa CUF ulipelekea Tanzania kuandika historia ya mauaji ya watu kadhaa kupitia jeshi la polisi hapo Januari 26, 2001 na wananchi wengine kukimbilia Ukimbizini Mombasa.
Leo ni Januari 8, 2015 na zimebaki siku 18 kufika Jauari 26 ambayo CUF huwa wanaiadhimisha siku ile (Januari 26&27). Lakini Januari 26 &27 ya mwaka huu itabeba sura ya kuadhimisha mauaji ya wafuasi wa CUF na pia ni tarehe ambayo itakuwa imetimia almost 3 months tangu ZEC ilipotangaza ingeitisha marudio ya uchaguzi baada ya miezi 3.
Swali kwa serikali na CCM, je mnafahamu Januari 26 & 27 ya mwaka huu itakuwa ni ya nini kwa CUF hususani huko Zanzibar? Itakuwa ni ya kurudia uchaguzi, itakuwa ni ya CUF kuadhimisha mauaji ya wafuasi wake ambayo yalisababishwa na kile kile kilichotokea kwenye uchaguzi wa mwaka jana au itakuwa ni tarehe ya kuadhimisha mauaji ya wafuasi wake na wakati huo huo kuwaambia wafuasi wao wadai haki yao kwa njia wanayoona inafaa?!
Angalizo ni kwamba, endapo ndani ya wiki mbili zijazo hakutakuwa na muafaka kati ya pande mbili basi CCM na serikali yake ijiandae kukabiliana na chochote kitakachotokea Januari 26 & 27 mwaka huu. Narudia, CCM na serikali yake wasidanganyike na utulivu uliopo Zanzibar hivi sasa; watu wanachosubiria ni tamko tu!