Wimbo
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 863
- 617
Barabara Nyingi za Lami zinapita sehemu za vijiji na miji, upo uhalibifu unaoweza kusababishwa na watu au matukio yasiyotegemewa kama mafuliko, lakini pia ufyekaji wa vichaka au miti inayoweza kusababisha ajali. Fedha Nyingi inapotea kuwalipa wakandalasi ati kwa ajili ya kufyeka nyasi, kazi ambayo ingekabidhiwa kwenye vijiji husika ingefanyika kwa wakati na kwa gharama ndogo, Hali kadhalika kufukua mifereji ili makarafati yapitishe maji bila shida. Hiyo fedha kama ipo ilipwe vijiji husika kwa ajili ya maendeleo mengine. Ninaupongeza uzalendo wako. Ni nawiwa kuunga mkono jitihada zako za kitukwamua.