mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Ni uungwana tu kama mheshimiwa Kikwete utaomba radhi kwa watanzania hapo kesho kwani ndio muda muafaka na nafasi pekee ya kufanya hivyo.
Omba radhi watanzania kwa kuifanya hii nchi kukosa mwelekeo na kuwa shamba la bibi. Mara nyingi tumemsikia rais Magufuli akilalamika kwamba hii nchi ililiwa sana, huko serikalini mambo yaliyokuwa yanafanyika yalikuwa ya hovyo, na akasema anaposema ya hovyo ni ya hovyo kwelikweli, kwamba hii nchi ilikuwa shamba la bibi.
Haya maneno ameyasema kwa kuyarudiarudia huyu unayemkabidhi madaraka ya chama leo.
Ili kuonesha basi unamuunga mkono mh rais na mwenyekiti mpya, na kwamba anayoyaongea ni kweli na si porojo za kisiasa, omba radhi. Usipofanya hivyo wenye akili zetu tutajiuliza mengi sana. Na tutaamini kwamba hizi ni mbinu za chama chenu kuwarubuni wstanzania.
Ama ukubaliane na Magufuli kwa kutuomba radhi watanzania au ukanushe kwamba hukufanya hii nchi shamba la bibi na tumbuatumbua inayoendelea ni utaratibu wa kawaida wa uongozi mpya kujipangia safu yao na si kweli kwamba ni wabadhirifu kama wanavyosemwa na mh rais!
Usipofanya hivyo basi wewe na chama chako mtakuwa mmewadharau sana watanzania na haya mnayofanya sasa yatakuwa ni maigizo tu!