Mheshimiwa Zambi anaendelea kulazimisha jambo ambalo ameishajibiwa na Waziri Mkuu kuwa linafanyiwa kazi. Analazimisha kwa vile aliyemtuma Bw. Kumburu(Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Kahawa) anaona mwisho wake unakaribia. Hivyo kwa maslahi ya Kumburu yuko tayari amlazimishe Waziri Mkuu avunje katiba ya nchi kwa kutoa amri ya kusimamisha utekelezaji wa sheria. Mh. Zambi anatakiwa kujua kuwa kuna utaratibu wa kufuata kufikia maamuzi ya kutengua kanuni na kwamba hatutegemei ataishinikiza serikali ivunje hizo taratibu.
Wote tunajua kuwa kupambana kote huko kwa mh. Zambi ni kumlinda Kumburu kwa vile kwa mdomo wake tarehe 24.05.2012 mjini Morogoro katika Mkutano Mkuu wa Wadau alimuhakikishia Kumburu kuwa asiogope atamlinda. Anataka kumlinda muhalifu ambaye amethibitika kutenda makosa. Serikali imekuwa inashindwa kumchukulia hatua kwa vile alikuwa amenunua Bodi ya Wakurugenzi iliyopita chini ya Bw. Pius Ngeze. Bw. Ngeze alikuwa amemwakikishia ya kuwa asihofu chochote kwa vile kiutaratibu Wizara ya Kilimo hata ikimkuta ana makosa hawana ubavu wa kumwajibisha bila ya kuandikiwa kwanza barua na Bodi yake. Maneno haya Bw. Ngeze aliyasema katika kikao cha Wafanyakazi katika ukumbi wa mikutano wa Bodi ya Kahawa Moshi. Hii pengine ndiyo iliyopelekea serikali kuweka Bodi mpya kwa kutumia vigezo vya kuteua wajumbe wasiokuwa na njaa na au kuendekeza njaa ili wasijenunuliwa na Kumburu.
Hatua za kwanza zilizoanza kuchukuliwa na Bodi hii mpya zinatia matumaini kama, kuamuru wafanyakazi ambao Kumburu alitaka kuwafukuza bila ya kufuata taratibu warudishwe kazini. Pia kumtaka aite kikao cha wafanyakazi wote ili kuondoa migongano na kujenga timu itakayoleta ufanisi kazini. Kitendo cha kuamuamuru Kumburu awarudishe kazini wafanyakazi ambao wanatofautiana naye kimtazamo kuhusu uendeshaji wa shirika la umma kukidhi maslahi yake binafs hakukubaliani nacho. Hivyo ili kutotaka kutekeleza maamuzi ya Bodi ya Wakurugenzi, kwanza akatumia visingizio mbali mbali asiite kikao cha wafanyakazi, alipobanwa akaendelea kumtumia mh. Zambi alete vurugu ili serikali ifute Bodi ya Wakurugenzi. Matumaini yake ni kuwa Bodi ya Wakurugenzi ikishafutwa hata maamuzi yaliyotolewa na Bodi hiyo yawe batili aendelee kuliendesha shirika la umma bila ya kufuata misingi ya sheria.
Hivyo vurugu anazofanya mh. Zambi zinadhaminiwa na Kumburu mwenyewe na pengine zinafadhiliwa na maboss wanaomtumia Kumburu mathalani ecom,café Africa,Technoserve, armajaro,Hanns neumannn na Solidaridad ambao wameunda mtandao wa kudaka kahawa ya Tanzania chini ya mpango utakao sajili kahawa ya Tanzania kama utz kwa kutumia pesa za Bill & Melinda Gates Foundation. Mtandao huu unataka kutumia vikundi vya wakulima. Hii ndiyo maana Kumburu akajiingiza kwenye kikundi cha Songea Network Center ili mgao wake upitie huko. Ushahidi ni kwamba Kumburu mwenyewe alishapelekwa kutembelea makampuni hayo au baadhi ya makampuni hayo na Café Africa miaka kama miwili iliyopita. Hata miezi kama miwili iliyopita alienda ujerumani kwa kisingizio cha kufuatilia maonyesho lakini nia kubwa ilikuwa ni kukutana na Padre kiongozi wa Kikundi chake cha Songea Network Center na maboss wa ecom kukamilisha mikataba.
Ili mtandao huu ufanikiwe wanapigana kuua masoko mengine ili wakulima walazimike kuwauzia kahawa wao kwa wale wasiokuwa wanachama na wana shida ya kuuza kahawa kutatua shida za dharura. Hii inatokana na uzoefu walioupata Technoserve katika kuendesha miradi yao Kaskazini. Miradi hiyo ilishindwa ushindani ikabidi Technoserve iisimamishe huko kaskazini, wakazanie Kusini huku wakimtumia Kumburu aondoe ushindani Kusini. Wakishinda kuondoa ushindani kusini ndipo warudie huko kwingine.
Kutokana na hali hii ni wazi suala la wajumbe wengi kutoka kaskazini siyo hasa linalomsukuma mh. Zambi kupambana Bodi ya Wakurugenzi ivunjwe. Nia hasa ni kutaka kumlinda Kumburu ambaye anaona dhahiri hawezi tena kutumia nafasi yake kwa maslahi binafsi.
Mimi naishangaa serikali kwa kushindwa kumwajibisha Kumburu kwa kutenda makosa yenye ushahidi wa wazi kama kuendesha Bodi kwa kutumia mfumo ambao haujaidhinishwa na serikali, kukihuka sheria ya manunuzi hadi Bodi ya kahawa ikaadhibiwa na PPRA, upotevu wa pesa za kuchapia makaratasi ya usajili wa wakulima, kunyanyasa wafanyakazi n.k. Nimeambatanisha dossier inayoonyesha makosa ambayo Kumburu amekuwa akiyatenda tangia amekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa. Watu wanajiuliza hivi serikali inamwogopa nini kumwajibisha mara moja huku yeye anaendelea kuwachafua viongozi wake.
Hivi serikali ilipompa kazi haikum- vet. Kama alikuwa veted hawakupata historia ya tabia yake ya mapambano jinsi alivyovuruga Mbinga Coffee Curing akipambana na aliyekuwa Meneja wake Bw. Kasongo. Baada ya kuacha amewavuruga ndipo alikimbilia Technoserve. Wito ni kuwa safari hii asiachiwe akimbilie sehemu nyingine kwenda kufanya uharibifu, tunahitaka serikali imfikishe TAKUKURU na kisha mahakamani ili awajibike kwa yote aliyoyatenda.
Mwisho niseme, Waziri kulingana na sheria ya kahawa anamamlaka ya kuteua wajumbe wa Bodi peke yake. Mwenyekiti uteuliwa na Mh. Rais. Kati ya wajumbe 8 walioteuliwa na waziri, wajumbe wanne ndio wanatoka mkoa wa Kilimanjaro na hata hao wajumbe imetokea tu wakatoka Kilimanjaro kwa vile waliteuliwa kuwakilisha taasisi ikatokea wakawa wanatoka mkoa wa Kilimanjaro, mathalani prof. James Terri anatoka Tacri(Taasisi ya utafiti wa Kahawa Tanzania), Bw. Ngimaryo antoka TCA(Tanzania Coffee Association) na biashara yake iko based Mbeya, Bw. Swai anatoka KNCU (Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro), Bw. Msuya anatoka serikalini ila anauzoefu wa kuongoza Bodi za Serikali. Na hii siyo mara ya kwanza kujikuta wajumbe wakatoka sehemu moja. Bodi zilizopita zilizonyingi wajumbe wake wengi walikuwa wanatoka mkoa wa Kagera. Mbona hatujawahi kusikia mh. Zambi akilalamika kuwa Mbinga yenye kahawa nyingi huko nyuma haikuwa na mwakilishi kwenye Bodi na sasa ina wawakilishi wawili.
Mh. Zambi kila mtu anaona wazi kuwa unazuia serikali isimwajibishe Kumburu.