Mhe. Zitto Kabwe: Asante Umetufungua macho!

Wanasiasa ni hatari, yaani ndo maana wakati wa uchaguzi wanamwaga rushwa kama hawana akili nzuri, pilau na wali kuwaonga wapiga kura, kumbe ni kwa maslahi binafsi.
 
Watu walafi wanaitafuna tu nchi bila kuangalia maslahi ya vizazi vya baadaye
 
Heading ya habari yako kuwa Tetesi siyo fair
 
Kwa hiyo mihela yote ya kodi wanaimaliza wao..bila hata kukatwa kodi...ama kweli siasa ni dhahabu kuliko ueledi wa fani nyingine yoyote hapa bongo.


Kwani ulikuwa hujuwi hili? Unafikiri kwanini kina Mulugo wana foji vyeti ili wapewe uwaziri? Sasa mtu kama Pinda ana umuhimu gani katika nchi hii mpaka aje kulipwa milioni 26 kwa mwezi?
 

Mkuu heshima yako. Naombe utuwekee na uwiano kati ya kima cha chini enzi za Nyerere na leo kwa J.K. Ndo tutajua nani mlafi.
 

Ahsante.. Ahsante..
 

Ina maana Mshahara wa Raisi upo chini zaidi ya Mkurugenzi wa TANROAD?? Mmmmmh Siamini hii kitu na kama ni hivyo ndio maana Safari za Nje haziishi
 

Haka KA Zitto KENYEWE KANAFIKI TU , MBONA HAKATAJI MSHAHARA WA MBOWE ? NA DR.SLAA? KAMA DR. ANANYAKUA HELA ZOTE HIZO NA BADO KAJIKOPESHA M140.. SI HATARI HIYO?
 
Last edited by a moderator:
sijui nani alinimezesha sumu kuna mtu alinidanganya raisi analipwa m8:
 
sijui nani alinimezesha sumu kuna mtu alinidanganya raisi analipwa m8:
Ninarudia, kama ni kweli Mhe. Rais na Waziri Mkuu wanalipwa hayo mamilioni ya walipa kodi bila haya na wanaona ni haki yao, hakika Mwenyezi Mungu atawalipa hapa hapa Duniani. Ni Roho ngapi za Watanzania wanateseka kwa sababu ya umasikini????? Mhe. J.K, hivi yanayosemwa ni kweli?
 
mungu tunamuongozea majukumu ambayo mengine sisi tunaweza kuyamudu sasa mshara wa raisi na mungu wapi na wapi lipo ndani uwezo wetu hili tukiamua upunguzwe inawezekana
 

mkapa yeye alikua analipwa sh ngapi????
 
Hivi mkapa mshahara wake ulikua ni sh ngap???

Je mshahara wa rais hua unapangwa na rais mwenyewe ndie anaejiamulia au ni nani anaehusika na kupanga kima cha mshahara wa rais?
 

Mkuu haya ni yakweli.ndio maana mpaka sasa si Pinda wala ikulu iliyokanusha zaidi ya kuwatumia Tughe kumtishia zitto.hasara sana kuwa na viongozi wa namna hii.
 

Hapo hujaumia zaidi bila kuambiwa kwamba mishahara hiyo ya Rais naWaziri Mkuu pamoja na Wabunge wao HAIKATWI KODI. Yaani hawalipi kodi. Kutokulipa kodi kwa hawa wakuu kuna maanisha kwamba ni wananchi pekee ndiyo wanaojenga nchi yao, hawa wasiolipa kodi wanaibomoa. Tusidanganyane kwamba eti kutokana na majukumu yao hawastahili kulipa kodi au kwa sababu yoyote ile. Kule Marekani ambako kila jambo tunajaribu kuiga, viongozi wetu hawataki kuiga kwa Rais wetu kulipa kodi kama Obama anavyolipa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…