Mhasham Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,948
32,056
2016%2B-%2B1

Kwa kiasi cha juma zima hivi mitandao ya kijamii imeweka picha hiyo hapo juu ya Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania, Mhashama Polycarp Pengo na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Picha imamuonyesha Kadinali Pengo akimfanyia maombi Bwana Makonda bila shaka akimuombea Mungu amuimarishe katika kazi yake mpya ili aifanye kwa ufanisi zaidi.
Paul Makonda amependa cheo kutoka Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hadi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Baadhi ya Waislam wameonyesha hofu kubwa katika tukio hili na nadhani hofu hii imetokana na dhana ya Mfumokristo katika serikali ya nchi yetu.

Binafsi nimeliangalia hili kwa jicho jingine kabisa nalo ni kuwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir keshafunguliwa njia na kiongozi mwenzake wa kiroho.

Kadinali Pengo kadhihirisha kuwa vitu kama hivi vya kuwaita watendaji wa serikali ofisini na kuwaombea Mungu vinaruhusiwa.

Mwito wangu kwa wale wenye hofu kuwa labda wataambiwa ''wanachanganya dini na siasa,'' ni kuwa waondokane na hofu hiyo na wasaidie kuwaondoa hofu viongozi wa Waislam ili na wao waige mfano wa Kanisa Katoliki.

Itapendeza siku moja kuona picha ya mtendaji Muislam yuko ofisini kwa Mufti wa BAKWATA Sheikh Abubakar Zubeir anasomewa Surat Yasin.

2016%2B-%2B1

Posted 1 hour ago by Mohamed Said
 
Unafiki tu huo.Hajawahi hata siku moja kwenda huko akiwa Mkuu wa Wilaya au alikatazwa???

Leo imekuwaje ameenda??
 
Mnafiki ni anayemuombea ambaye wakati watu wanadhulumiwa huko Zanzibar alikaa Kimya. Halafu ndugu yangu Mohamed Said hata huyu Mufti naye ingawa si mfumo Kristo lakini ni mfumo CCM. Hao wote wawili wamekaa kimya kama vile CCM haidhulumu watu au kuvunja haki za binadamu. Ndiyo maana huko ulaya watu wengi sana wanaamini kwamba hakuna mungu.

Yale matamasha ya kuombea amani umewahi kuona watu toka vyama vingine wakialikwa!?
 
Allen Kilewella: kwa jina lako hilo naamini ni mfuasi wa Kristo. Kama ni hivyo soma naisha yake Kristu Agano Jipya jinsi alivyotumia muda wake kurudisha kondoo waliopotea kundini. Hiyo ilikuwa ni kazi ya moja zilizomleta duniani.

Pili, kutumia neno "mnafiki" kwa kiongozi Mkuu wa Kanisa ni kuwatukana waumini wote wa kanisa hilo. Sijui kama una hata chembe ya sifa alizo nazo huyo kiongozi wa dini, katika katika kila hali na nyanja zote za maisha kama binadamu.

Huwe unachagua maneno ya kuandika. Na ninaamini hapo ulipo roho yako ilikusuta baada ya kuwa umeruhusu andiko lako liende. Achana na ujana bali ishi kijana.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
 
Allen Kilewella

Kwamba anachofanya Pengo kumbariki Makonda hayo ni mambo ya kiimani, lakini kwa mtu anayetaka kuonekana ni mtumishi wa mungu yuko kimya kwa watu kudhulumiwa haki yao na anakaa na waliodhulumu bila ya kuwaambia kwamba wamedhulumu, huo ni unafiki!!
 
Jikumbushe tafsiri ya unafiki au tupe tafsiri yako na siyo kwa mfano huo. Nafasi ya Kiongozi wa Dini ni tofauti na ya kiongozi wa utawala. Tofauti kubwa ni matokeo (results) ya kazi zao. Wa utawala matokeo hupimwa kwa mizani za maisha, ambako wewe unaegemea - ati amekaa kimya! Hudhuria mahubiri yake, au pata machapisho yako kabla hujamwita "mnafiki". Sintokosea kukuita wewe MNAFIKI mkubwa wa FIKRA na FIKARA.

CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA.
 
Sala za mashekh ataziweza?
Kila mtu na Imani yake bhana!

Na ni utaratibu wa Kikristo pale unapokutana na kiongozi wa kiroho kuombewa bila kujali ni kanisani, nyumbani au hata barabarani!

Naona weingine ibada lazima iwe kwenye mazishi na kwenye nyumba ya ibada tu!
 
Kwamba anachofanya Pengo kumbariki Makonda hayo ni mambo ya kiimani, lakini kwa mtu anayetaka kuonekana ni mtumishi wa mungu yuko kimya kwa watu kudhulumiwa haki yao na anakaa na waliodhulumu bila ya kuwaambia kwamba wamedhulumu, huo ni unafiki!!
Wewe unatumia kipimo gani kufahamu kama wamedhurumiwa haki yao na unafahamu na yeye anatumia kipimo gani kufahamu kama hawajadhurumiwa haki yao?

Kwani kazi ya Pengo ni kutoa haki? Kwani Mahakama hazipo?

Nadhani tatizo lako unachofikiri wewe unataka na wengine wafikiri hivyo hivyo?

Haya ni mawazo au fikra za kidikteta!
 
In General viongozi wa dini hapa Tanzania wamekuwa wanafiki sana, Waumini wao wako kwenye mateso makubwa kutoka kwa watawala, lakini viongozi hawa ndio wamekuwa mstari wa mbele kujipendekeza kwao!
Nilichukizwa sana na wale viongozi wa dini waliokuwepo jana pale uwanjani kwenye hafla ya kuapishwa SHEIN.
 
Jikumbushe tafsiri ya unafiki au tupe tafsiri yako na siyo kwa mfano huo.
Mnafiki ni yule mtu ambaye anajua jambo lakini anajifanya kama alijui au ana msimamo ambao hataki kuuonesha hadharani ingawa matendo yake yanasawiri msimamo wake huo. Maaskofu wa Katoliki walikubaliana nini kuhusu Katiba mpya na Pengo alifanya nini kama si unafiki?
 
Allen Kilewella: kwa jina lako hilo naamini ni mfuasi wa Kristo. Kama ni hivyo soma naisha yake Kristu Agano Jipya jinsi alivyotumia muda wake kurudisha kondoo waliopotea kundini. Hiyo ilikuwa ni kazi ya moja zilizomleta duniani.

Pili, kutumia neno "mnafiki" kwa kiongozi Mkuu wa Kanisa ni kuwatukana waumini wote wa kanisa hilo. Sijui kama una hata chembe ya sifa alizo nazo huyo kiongozi wa dini, katika katika kila hali na nyanja zote za maisha kama binadamu.

Huwe unachagua maneno ya kuandika. Na ninaamini hapo ulipo roho yako ilikusuta baada ya kuwa umeruhusu andiko lako liende. Achana na ujana bali ishi kijana.

TAFAKARI CHUKUA HATUA.
Kuna kitu anakitafuta huyu bwana.
 
Mimi mahali ninapoona tatizo ni kwenye picha tu, nikiona mtu amefanyiwa maombi huku ameendaa wapiga picha nakuwa naona kama ni show off tu, hakuna jingine.
Kuombewa ni jambo zuri ila kuita mpiga picha hizo ni show off tu ndo alipoharibu labda angeiweka kwa matumizi binafsi hata bwana Yesu huwa hapendi show off hupenda moyo mnyoofu, tena hata ukifunga unatakiwa usijionyeshe kwa watu. Makonda apunguze show off huyu sijui ni mtumishi wa ngapi anapiga naye picha ki hivo
 
Anataka kufunika nini?
 
Jamaa mbwembwe nyingi, kila akienda kwa mtumishi anapiga picha. Sasa hayo ni maombi au ni picha tu.

Hata concentration inapotea kwa kuwaza picha imetokaje, tena ukute walikuwa kabisa wanajadili jinsi picha ilivyitoka vizuri.
 
Maombi ya kweli hayahitaji maandalizi ya picha hapo kwa wenye uelewa mdogo tayari wata create different meaning. Sasa yeye sijui alilenga nini. Yani maombi na camera loh hii hatari awamu hii viongozi wanapenda camera ka kina kardashians
 
Back
Top Bottom