KWA mara nyingine tasnia ya habari nchini imepata pigo la kuondokewa na Mhariri
Mkuu wa gazeti la kila siku la Jambo Leo, Willy Edward (38), aliyefariki ghafla
usiku wa kuamkia jana akiwa mjini Morogoro.Taarifa za kifo chake zilitolewa na mhariri mwenzake wa gazeti la Mtanzania,
Kulwa Karedia, ambaye alikuwa naye kabla ya kufikwa umauti, akisema kuwa alikuwa
ni mzima wa afya, na kwamba aliwaaga anakwenda kuwaona watoto wake ambapo alikaa
huko mpaka saa 6:30 usiku.
Alisema muda wa kurudi hotelini alikokuwa amefikia ulipofika, Willy alimwita
dereva wa pikipiki ili amchukue, lakini usafiri huo ulipofika hakuweza kuupanda
kwani alipotoka nje na kutembea kwa hatua chache alianguka.
Karedia aliongeza kuwa, ndugu zake walimkimbiza hospitalini na baada ya
vipimo vya daktari, ikabainika kuwa alikwishafariki dunia
HABARI ZAIDI ANGALIA TANZANIA DAIMA