Mhandisi Kundo afanya kikao kazi na watendaji Sekta ya Maji

Mhandisi Kundo afanya kikao kazi na watendaji Sekta ya Maji

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
158
Reaction score
103
Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa, Mhandisi Andrew Kundo (Mb) amekutana na watendaji wa sekta ya maji Mkoa wa Dar es Salaam, Ma
WhatsApp Image 2026-03-04 at 17.01.55.jpeg
mlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) katika kikao kazi kilicholenga kupata taarifa ya hali ya utoaji huduma ya maji mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Akizungumza katika kikao kazi hicho, Mheshimiwa Kundo amewapongeza watumishi wa DAWASA kwa kazi nzuri ya kutoa huduma ya maji kwa wananchi huku akisisitiza kuongeza ubora katika kuhudumia wateja na mapambano dhidi ya upotevu wa maji.

"Tunapoboresha huduma kwa wateja tutaondoa kabisa malalamiko ya wateja hata kipindi cha changamoto, niendelee kuwatia moyo kwa kazi nzuri mnayofanya na niwahakikishie wizara ipo pamoja nanyi wakati wote," amesema Mhandisi Kundo.

Mheshimiwa Kundo ameitaka DAWASA kuongeza kasi katika swala la uwekaji wa dira za malipo ya kabla (pre-paid meters) kwani uwekaji wa mita hizo ni agizo rasmi la Mheshimiwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona huduma ya maji inaboreshwa kwa wananchi.

Aidha, Mheshimiwa Kundo amesema swala la upotevu wa maji lishughulikiwe kwa wakati kila mara inapopokelewa taarifa ya upotevu wa maji ili kupunguza hasara inayotokana na upotevu huo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DAWASA, Mhandisi Romanus Mwang'ingo amesema Mamlaka inaendelea kupambana na swala la upotevu wa maji na kwasasa ipo mbioni kukamilisha mpango wa kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema DAWASA imejipanga kushirikisha wadau hasa sekta binafsi ili kuhakikisha shughuli za Mamlaka zinakwenda na wananchi wanapatiwa huduma ya maji.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja, CPA (T) Rithamary Lwabulinda amesema Mamlaka imeendelea kujipanga vyema katika swala la ufungajj wa dira za malipo ya kabla na kwa mwaka wa fedha 2025-2026 Mamlaka itafanya manunuzi ya dira 65,000 na kuanza kuzifungula kwa wateja.​
 
Pelekeni habari zenu Facebook huko huku mmefikaje na hakuna access ya kupafikia ina maana nyie ni wahaini na mnavunja sheria kwa kutumia VPN kinyume na sheria na mnatumia mtandao uliofungiwa na hao viongozi wenu vilaza kutuletea taarifa humu
Shabhaaaash
Moderator pigeni bani vitaasisi na viasasi vya kiserikali humu hatutaki upuuzi hapa kama wataka kuleta habari waifungulie JF
Maxence Melo
 
Back
Top Bottom