YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,902
- 51,994
Muhadhiri wa Chuo cha Diplomasia Bw. Innocent Shoo akihojiwa na sauti ya Amerika jana usiku alichemka pale alipomtaka Raisi Magufuli aingilie kati mgogoro wa uchaguzi Zanzibar.
Kama Mhadhiri wa chuo cha Diplomasia alitakiwa asome Katiba ya Tanzana inavyosema kuhusu uwezo wa rais wa Muungano unaishia wapi.
Mambo ya uchaguzi wa Zanzibar si mambo ya Muungano hivyo Rais wa Muungano hawezi yaingilia kwani katiba haimuruhusu akiingilia anakuwa kavunja katiba
Pili ZEC ni tume huru.Na hakuna Rais awe wa Zanzibar au MUUNGANO MWENYE uwezo wa kuingilia tume ya Uchaguzi iwe NEC au ZEC kwa sheria za hizo tume za uchaguzi
Ninawashauri wataalam wetu wakiongea na vyombo vya habari vya kimataifa wawe makini na wawape taarifa sahihi na ndio maana wanawafuata wao kama wataalamu.