Mh. Suzanne Kiwanga mbunge wa Jimbo la Mlimba, umeme utawashwa lini vijiji vilivyobaki?

Mbingu

Member
Jun 8, 2015
27
6
Mh Mbunge wa Jimbo la Mlimba tupe majibu umeme kuanzia Njagi, Mbingu, Kisegese na Idete utakuwa umekamilika na kuwashwa lini manake toka mwaka jana tunaona nguzo zimesimama na waya tayari zimeshamesha fungwa ila hakuna kinachoendelea.

Nakufuatilia unapokuwa bungeni kuchangia hoja sijasikia ukigusia hilo, vipi unaona 2020 mbali sana?

Sasa wewe endelea kujisahau zawadi yako utaipata tumechoka maisha ya giza.
 
Hilo ni jukumu la Serikali sio mbunge, mbunge anaweza kukumbushia kwa maandishi au kwa kuuliza moja kwa moja lakini huwezi kumsikia kwa sababu hakuna bunge live
 
Kwa hiyo sisi tuliopo jimboni kwake tunapataje taarifa kuwa huu umeme unawaka lini? Tusaidie mkuu labda uelewa wangu mdogo
 
Umeme vijiji vilivyobaki utawaka baada ya kitambo ingawa si rahisi kwa vijiji vyote kuwa na umeme kwa hivi karibuni
 
Umeanza matusi, ndiyo tabia yenu uvccm mkishindwa hoja mnakimbilia matusi
Mimi sikutukani ila ww nadhani ujui kazi ya mbunge Jimboni kwake sasa kama tatizo la umeme tuwaulize tanesco, na hii barabara tuwaulize Tanroad sasa mbunge anatuwakilisha kwa lipi? Wakati yeye ilitakiwa atusemee then atupe mrejesho wa majibu kutoka serikalini, ila kama unaleta uchama kwenye ilo jambo kama vile nyinyi chadema nyumba zenu zina umeme poa.
 
Tatizo la watanzania wengi tunawaamini wanasiasa, sasa nikwambie kitu mkuu mbunge wa ccm walikaa toka uhuru kwenye jimbo lenu na walishindwa kuweka huo umeme, na huyo wa cdm akishindwa tafuteni wa chama kingine ila msirudi ccm wala cdm kwani wao wameonesha kushindwa tayari
 
Na ndoma tukawanyima ubunge 2015-2020 tukampa kutoka cdm lakini michakato hiyo ilianza kabla ya huyo kuchaguliwa ila wakati anajinadi nadhani aliaidi umeme ungewaka mwaka jana mwishoni sasa tunamuuliza atupe majibu tatizo nn? Hizo habari za wabunge wa ccm toka ukoloni mi haziniusu mkuu tunaitaji umeme kwa sasa.
 
Mh Mbunge wa Jimbo la Mlimba tupe majibu umeme kuanzia Njagi, Mbingu, Kisegese na Idete utakuwa umekamilika na kuwashwa lini manake toka mwaka jana tunaona nguzo zimesimama na waya tayari zimeshamesha fungwa ila hakuna kinachoendelea.

Nakufuatilia unapokuwa bungeni kuchangia hoja sijasikia ukigusia hilo, vipi unaona 2020 mbali sana?

Sasa wewe endelea kujisahau zawadi yako utaipata tumechoka maisha ya giza.
Nakushauri huu uzi wako hamishia kwa user huyu wa JF
TANESCO
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom