Mh Raisi wangu Magufuli TCRA si wakweli watupiwe jicho,walidanganya kuhusu computer mashuleni

Alatuhiga

JF-Expert Member
Jan 4, 2015
523
79
Hawa jamaa wa TCRA kiukweli ni wa sanii.Walitoa ahadi kuzisaidia shule kadhaa computer kama shule 12 hivi zaidi ya mwaka mmoja sasa,hawajatoa hata moja.

Shule zilituma walimu wao kwa gharama kubwa kupigwa msasa na kisha wakawaita wakuu washule na kuita vyombo vya habari kushuhudia kukabidhiwa kwa computer wakaleta sample za hizo computer na kisha kuambiwa watangulie zita kuja.

Hakuna hata computer moja iliyo pelekwa kwenye shulehe hata moja.Kabla kidogo ya uchaguzi mkuu,walipo ona watu wanasemasema,kwa kuhofu isiwe tatizokwenye kampeni wakatuma watu kwa kile walicho ita kukagua vyumbana kuahidi kuzileta baada ya siku mbili tatu.Mpaka leo hamna kitu.Jamani nchi hii ita endeleaje Kwa usaniikama huu.

Kwanini kusumbua watu kama mlikuwa hamna computer.

Huenda zilisha chukuliwa na wajanja.Nchi hii kilamtu ni mpigaji wa hela tu.Mh.Rais ebu mulika wasanii kama hawa.Tukipata niafasi ya kuwasiliana na mh.Maguli tuta lisema hili.

Kwanini watu waseme wana computer kumbe hawana?Kwanini kujionyesha una kitu kumbe huna?
 
TCRA kuna wasomi wazuri wa Tehama,tuambieni kilicho tokea vinginevyo tutajua ni mpango wa makusudi kutu danganya watu wa zima
 
Back
Top Bottom