Frey Cosseny
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 1,984
- 1,405
Yaani tunataka shule za serikali zinafanye vizuri wakati mawaziri,watunga sera,wakaguzi wa elimu,maafisa elimu ,makatibu wakuu wengi watoto wao hawasomi shule za serikali,ikiwa watendaji na wasimamizi wakuu wa shule za serikali hawafikirii kuwapeleka watoto wao shule za serikali msitarajie hata siku moja kuona shule za serikali zinarejesha makali yake!.
Ukitaka shule za serikali zirejeshe makali yake,leo Rais aseme ukiwa mtendaji mkuu serikalini peleka watoto wako shule za serikali.
Viongozi na watendaji wakuu wa serikali miaka ya tisini walikuwa wanaona fahari kuona watoto waonwakisoma Umbwe boys,Tisamaganga,Kazima,Mwanza Sec,Azania,Jangwani,Mwenge,Milambo,Mzumbe ,Pugu,Kilakala,Shycom,Msalato,Tanga Tech.
Leo wakubwa hawa hawawezi peleka watoto wao Tambaza,wala Jangwani,wanapigana vikumbo Kaizerege,Feza,Marian Girls n.k.
Fanya utafiti kuanzia katika departmental level,interministrial commetee,cabinet mpaka bungeni ujue watoto wangapi wa waliomo humo wanasoma shule za serikali!.
Ikiwa 95%ya wajumbe wa interministrial commetee ambao ndiyo think tank ya nchi,ndiyo inayoamua nchi ielekee wapi,watoto wao hawapo Kazima,Jangwani,Azania,Mzumbe,N.k,unategemea kuona shule za serikali ndani ya kumi bora?thubutu,utazikuta mkiani huko!.
Unategemea shule za serikali zinafanye vizuri wakati asilimia 80 ya walimu wana stress za kodi ya nyumba?zamani shule zilikuwa na nyumba za walimu,nakumbuka marehemu baba yangu marehemu Mwalimu Peter toka akiwa Kazima Sekondari mkoani Tabora,aalikuwa kwa nafasi yake shuleni alikuwa kwa wiki tunaona nyama zinaletwa nyumbani kama motisha kwa wakuu wa shule na wasaidizi wao!.
Tukiwa wadogo nilishuhudia jinsi walimu wale wa Kazima alipokuwa marehemu baba yangu,Milambo,Tabora boys,Milambo,Tabora Girls,walivyokuwa na furaha na kazi ya ualimu,nyumba nzuri,mwalimu alikuwa haangaiki sehemu ya kuishi.
Leo nenda katembelee shule zetu,walimu hawana makazi,wanalalamika kupandishwa madaraja,mishahara haikidhi ukali wa maisha,leo hata wao baadhi hawawasomeshi watoto wao shule za serikali kwa sababu wanajua udhaifu wa shule za serikali walizopo!.
Elimu inahitaji uwekezaji mkubwa,kama tunataka shule za serikali zifanye vizuri,lazima turejeshe mazingira ya shule yaliyokuwa miaka ya 90 kurudi nyuma,kazi ya ualimu ni taaluma nyeti,haitaki ubabaishaji wala blabla,lazima tuwekeze sana,maslahi ha walimu lazima yatiliwe mkazo!.
Bila walimu bora wenye morali,mazingira bora ya kufundishia,miundombinu bora,shule za serikali katu haziwezi kurejea kwenye ubora wake!.
Inasikitisha kuona leo uwekezaji kwenye elimu umekuwa ukizingwa na vijembe,badala ya kuzungumzia uhalisia,dhamira ya dhati ya kuifanya elimu kuwa bora inasuasua!
Tuungane kwa pamoja kuzirejesha shule zetu za serikali katika makali yetu!.
Anaandika Dotto Bulendu