bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,682
Ni takribabi mwezi taifa lina shudia matukio ya simanzi kufuatia vifo vya kikatili na unyama wa hali ya juu.
Tumeona watu 7wakichinjwa wilaya Sengerema, tukaishia kusikia watuhumiwa wamekamatwa, jijini Mwanza watu 3 wakachinjwa tukaishia kusikia taarifa za kukamatwa watuhumiwa, jijini Dar es salaam familia ikatetezwa ndani usiku wakiwa wamelala hatujasikia kinachoendelea, MDADA Annet kachinjwa jijini dsm tunasikia watuhumiwa wanasakwa, Tanga Amboni watu 8 wachinjwa, haya ni maelezo mafupi ya matukio ya kutia simanzi.
Tuache hayo nirudi katika suala nyeti la mauaji yenye sura ya kigaidi, nasema ni matukio yenye sura ya kigaidi kwasababu zifuatazo; moja mauji ya mwanza msikitini na Tanga Amboni ni dhahiri kuwa ni ugaidi kwa maana ya tafsiri ya ugaidi.
Takribani mwezi na nusu tangu itolewe video ya watu/vijana walio jinasibu kuwa wao ni wafuasi kikundi cha kigaidi cha ISIS hili jambo lilichukuliwa kimzaa sana, ila sasa naona tutaamini jinsi trendi ya matukio inavyoenda. Kibaya hapa ni kuwa kusubili mpaka matukio ambayo yanaambatana na kupoteza maisha ya watanzania ni jambo la hatari na kusikitisha kwa serikali inayojinasibu kufanya kazi kwa kasi.
Narudia kauli yangu hapo juu kwenye kichwa cha habari kuwa mkuu wa mkoa Tanga Martini Shigela anatakiwa kufukuzwa kazi. Naomba rais Magufuri kwa kuwa umekuwa ukionesha hasira dhidi ya watendaji wazembe natagemea kuona ukichukua hatua. Baada ya video kutolewa siku chache baada ya watu walewale wanao jinasibu kuishi kwenye mapango ya Amboni ni Martini Shigela aliyetoka kifua mbele akitoa taarifa kwa umma kuwa hakuna magaidi bali matukio hayo ni ya kiaarifu tu. Na baada siku chache watu wanachinjwa kama kuku maeneo hayo. Hili siyo jambo dogo la kuendelea kuwalea watu wanaotakiwa kuchukua wakifanya uzembe na kugharimu maisha ya watu. Shigela kama mkuu wa mkoa wa Tanga na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa anastahili kuwajibika na watendaji wake hasa mkuu kitengo cha intelijensia mkoa.
Pia nikuombe mh.rais angaza vyombo vyetu vya usalama, hasa kitengo cha usalama wa taifa na jeshi la polisi kuna mwanya/ufa ambao kama hautazibwa yatatokea makubwa kwa taifa letu hasa kwa usalama wa nchi na wananchi.
Natoa ushauri haya yanayotokea nasema ni matokeo ya viongozi wasio na ujuzi wala weledi wambo ya kiusalama maana matukio mengi yaliyotokea yangeweza kuzuilika kama tungekuwa na utendaji wa vyombo vya usalama maana kwa tukio la mwanza na tanga ni dhahiri kulikuwa na pre information za kuanzia kuzuia matukio. Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa polisi na idara nzima ya usalama wa taifa naweza kusema ni dhaifu maana kwa mkitadha matukio yenye sura za ugaidi yanafanyika kwa mbinu hafifu ambazo pia wameshindwa kukabiliana nao.
Nitoe ushauri km raia ila mwenye uwezo na akili ya kuangaza issues za usalama wa nchi licha yakuwa sina utaalam wa mambo ya kiusalama kwa maana ya kusomea ila kwa muda mwingi ninao utumia kufuatilia mambo haya ya usalama wa nchi ninazo sababu za kusema udhaifu huu wa vyetu vya usalama. pia niseme kuwa udhaifu wa vyombo hivi umetokana na mtandao wa kufanya idara hizi kuwa za kiukoo zaidi kwa maana ya watu wengi kwenye idara hizi wanapatikana kwa kutegemea mnyororo wa watu waliowahi kufanya kazi katika idara hizi. Ipo mifano mingi naamini ata wewe mh. Rais unajua kabisa utaratibu wa ajira katika jeshi la polisi na idara ya usalama zimekuwa zinatolewa kwa namna ambayo ina sura na dalili za kindugu(nepotism).
Shida nyingine ni utaratibu wa kupatikana viongozi wa idara hizi kutoka ngazi ya kitaifa kuteremka chini kuongoza idara hizi kwa kiasi kikubwa wanapatikana si kwa ufanisi wa kazo na historia ya utendaji kazi wao bali inategemeana na UNAMJUA NANI kati watu wanao teuwa wahusika.
Binafsi niseme kuwa nilikuwa na ndoto na hamu sana tangu nikiwa mdogo kufanya kazi na idara ya usalamq ila kila juhudi ziligonga mwamba sikwasababu sina vigezo bali sikuwa na mtu wa kunisaidia kuingia idara hii.
Nimalizie na kukuomba mh. Rais angaza vyombo hivi na pia fanya mabadiriko makubwq kuokoa hali ya usalama wa nchi wananchi unaoelekea kuyumba. Ni mwaka jana mashirika ya habari ya kimataifa yalitaja kuwapo mtandao wa ugaidi Africa mashariki hasa maeneo ya Kenya na Tanzania kwenye miji ya Mwanza, Tanga na mikoa mingine taarifa hizi zilipuuzwa naseme kauli moja, KWA MWANAUSALAMA BORA HATAKIWI KUPUUZA TAARIFA ASIYOJUA CHANZO CHAKE NA UKWELI WAKE.
Tushirikiane kulinda taifa letu, tusije kuwa kama nyani wanaochekelea msitu ukiungua wakasahau usiku waja ni watahiji kijihifadhi..