Mh.Rais Magufuli, waliotimuliwa kwa kashfa ya vyeti feki wapewe japo mafao yao, ni jasho lao halali

Aman Ng'oma

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
961
533
Kichwa changu huwa kinawaza sana. Lakini uwazaji wake ni tofauti kidogo. Najaribu kutazama mambo kwa upande wa pili japo si kwa nia mbaya bali kwa lengo la kutafuta amani ya nafsi na si nafsi yangu bali nafsi za waliyokutwa na maswahibu kadhaa wa kadhaa.

Serikali ya awamu ya Tano inapiga kazi ile mbaya tena kwa kasi kubwa, usipofunga mkanda wako vizuri unaweza ukajikuta umetupwa nje kabisa ya gari na kubaki ukishangaa tu pasi kujua ilikuwaje hadi ukatupwa nje.

Natambua watu wengi bado hatujapata kumwelewa vizuri Rais wetu Dkt. John Pombe Jeseph Magufuli, hata mimi binafsi nilikuwa napata tabu kidogo kumwelewa. Kwa kweli nilikuwa namwona kama Rais anayeivuruga tu nchi lakini kumbe sivyo, nilikuwa nimepotoka. Kuna wakati nilianza hata kujilaumu kwa kumchagua yeye, na hapa niseme tu ule ukweli wangu, kura yangu Rais aliipata lakini wagombea wengine wa ccm sikuwapa kwa maana kwamba nilitengeneza kura yenye macho. Kura yenye macho msingi wake ni kuwa katika uchaguzi, hakiangaliwi chama bali anaangaliwa mtu. Na ndivyo nilivyofanya mimi katika uchagu mkuu uliyopita. Sikuwa naangalia chama bali nilikuwa naangalia mtu. Mtu niliyeamini anakichwa kizuri, kwa maana kichwa chenye akili iliyotulia ndiyo niliyempigia debe na kumchagua. Hapa simaanishi kuwa wengine hawakuwa na akili iliyotulia bali nilikuwa napima kutokana na upeo wangu.

Kwa upande wa Urais, kichwa nilichokiona kinafaa kuongoza nchi hii na kuweza kuivusha salama ni Dokta John Pombe Magufuli. Hili nalitamka wazi sije nikaonekana kama ni mkosoaji wa mambo mazuri yanayofanywa na Serikali kwa nia njema. Tatizo kubwa ninaloliona kwa Mh. Rais hadi ashindwe kueleweka ni upeo wake mkubwa wa kuyatazama mambo, lakini vilevile shauku aliyokuwa nayo ya kutaka kuiona Tanzania ikipiga hatua kimaendeleo katika kila nyanja. Lakini vilevile ile hulka yake ya kutotaka mchezo mchezo kwenye utekelezaji wa majukumu ya umma. Jambo lake analopanga lifanyike lazima lifanyike tena kwa wakati. Watu wengi hatujazoea mabadiliko ya ghafla lakini Rais wetu amejaribu kutuonyesha kuwa mabadiliko ya ghafla yanawezekana, na kwamba tumechelewa sana. Kwa hali ilivyo lazima tukimbie mbio badala ya kuendelea kutembea. Anahitaji tuwakute wenzetu waliyotangulia na ikibidi tuwapite kwakuwa nchi yetu ina kila kitu na kwamba hakuna kitakacho tufanya tushindwe kupiga hatua.

Rais Dkt. Magufuli ni kiongozi asiyekubali kuyumbishwa na anayetaka nchi iende mbele. Mara nyingi amekuwa akitamka hadharani tena kwa kurudia rudia "nataka nchi iende atakayejaribu kunikwamisha, atakwama yeye". Haya ni maneno mazito sana kutamkwa na kiongozi wa juu kama yeye. Ni maneno aliyoyatamka kwa kumaanisha hasa, hana subira hata kidogo na watu wanaoleta mchezo mchezo kwenye mambo ya msingi. Je ni akina nani hao wanaoleta mchezo mchezo kwenye mambo ya msingi? Ni wale wote waliyofumba macho wasiyoona mazuri yanayofanywa na Serikali. kila jambo linalofanywa zuri linapotoshwa. Lakini wengine hugeuka kizingiti katika utekelezaji wa mambo ya maendeleo.

Kikubwa ambacho tunapaswa kijifunza ni kuwa wakati mwingine unapotaka kufanya jambo la maendeleo kuna watu watakukatisha tamaa, wengine watakubeza lakini wengine watatengeneza figisufugisu ili ukwamishwe kwenye utekelezaji wa majuku yako. Lengo lao kubwa waone umefeli mwisho wa siku wapate pa kusemea kuwa pamoja na kwamba una kila kitu lakini umeshindwa kuleta maendeleo yanayonekana machoni kwa watu.

Hapa kuna kitu muhimu tunapaswa kujifunza, ikiwa unataka kufanya jambo lolote la maendeleo na huku ukiwa umejiridhisha kuwa ufanyacho ni sahihi na kwamba kitakuwa na manufaa kwa sehemu kubwa ya jamii au kama ni mtu binafsi ukachuja wazo lako na ukaona ukilifanya litakulipa, wewe lifanye usisikilize maneno ya watu kwani siku zote miluzi mingi humpoteza mbwa, lazima uepuke kupotezwa na kuelekea kwenye uelekeo usiyoukusudia na hiki ndicho Mheshimiwa Rais anachokiogopa na kujitahidi kuchukua tahadhari mapema ili asiingie kwenye mtego wao.

Kimsingi mawazo ya Rais Magufuli ni makubwa sana. Inahitaji nawe uwe na upeo mkubwa ili uweze kumwelewa. Wakati sisi tunaitazama Tanzania sasa, yeye anaitaza Tanzania ya miaka ishirini ijayo. Ni matumaini yangu kuwa siku moja tutampigia makofi kwa kazi kubwa anayoifanya sasa. Huyu jamaa, bwana mkubwa, mwenye nchi ana uthubutu, si mwoga wa kuchukua maamuzi mazito na magumu yenye kuhatarisha hata usalama wake, kitu anachokiangalia zaidi ni maslahi ya taifa kwanza. Kitu chochote chenye maslahi makubwa na taifa huwa hawezi nyamaza kimya akabaki akiangalia tu watu wakicheza nacho, analala nao mbele wote . Na kwa namna anayofanya maamuzi ni kama mtu wa hovyo hovyo lakini ndiyo hivyo anapasua anga anakwenda na tayari sasa hivi tumekwisha kuanza mwaka wake wa pili na kila kitu kinaenda sawa.

Tumeshuhudia sakata la wafanyakazi wenye wenye vyeti visivyo halali zaidi ya elfu tisa na mia tisa wakitumbuliwa na wengine zaidi ya elfu moja na mia tano waliyokuwa wakitumia cheti kimoja zaidi ya mtu mmoja nao wakisimamishiwa mishahara yao hadi hapo itakapobaini rasmi ni nani hasa muhusika halisi wa cheti husika.

Binafsi naunga mkono zoezi hili kwani linarudisha heshima ya taaluma nchini. Inaleta umuhimu wa watu kukaa darasani lakini vilevile inaondoa ujanja ujanja wa watu wanaopenda kunufaika bila kutoa jasho na siku zote watu wa namna hii mara nyingi japo siyo wote huwa wanakuwa wasumbufu sana sehemu za kazi. Nchi ili iendelee lazima ipate watu wenye sifa katika kila nyanja. Lakini pia wawe wazalendo na wanaojituma katika kazi.

Hata hivyo, twende mbele turudi nyuma, lakini lazima tukubali tatizo limetokea. Pamoja na kuajiriwa kwao kumetokana na vyeti vya kufojiwa, vyeti visivyo halali, lakini bado watu hao ni watanzania wenzetu. Wamelitumika taifa hili kwa uadilifu mkubwa kabisa katika kipindi chote mtu alipokuwa kazini kabla ya kukutwa na majanga hayo. Tunapaswa tulitazame hili katika jicho pevu. Sote tunakubaliana walifoji vyeti, lakini pamoja na kufoji huko, josho lao lilitumika katika shughuli za uzalishaji na kulijenga taifa hili. wengi wao walifoji cheti cha kidato cha nne lakini katika ngazi nyingine walisoma. Kupitia kusoma huko walipata maarifa na ujuzi wa moja kwa moja ambao ulitumika katika kusaidia juhudi za kulijenga taifa hili. Tunapaswa tuwafikiriae tusiwafukuze kama mbwa.

Kuna ile michango yao katika mifuko ya hifadhi ya jamii, lile ni josho lao halali hawakumwibia mtu. Walifanya kazi zote kama alivyotaka mwajiri na wala haijapatapo kusikika kuwa mtumishi huyo aliyefoji cheti alipokabidhiwa majukumu na mwajiri wake alishindwa kuyatekeleza. Toka siku yake ya kwanza alipoteuliwa kuanza kazi, aliendelea kutekeleza majukumu yake hayo vizuri hadi alipokutwa na hatia hiyo.

Ushauri wangu ni Kuwa pamoja na kwamba wamefutwa kazi kwa kosa la udanganyifu, busara itumike. Walipwe yale mafao yao yote kwani lile ni jasho lao. Wapatiwe ili wakaanze maisha mapya na kutokea hapo udhibiti mkubwa ufanyike ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena.

Aman Ng'oma
Mwanza
0767989713
 
Sasa namba za simu za nini? Unahisi utatafutwa kwa ajili ya hichi ulichoandika? Not to that extent...
 
Wenye vyeti feki HAWANA haki ya kupata hata senti 5. Ajira zao hazikuwa halali. Haramu haiwezi zaa halali.

Mkataba wowote walio saini na serikali kwa vielelezo vya kugushu umekuwa batili. Kama ulitowa kauli ya uwongo, unachokipigania sio halali yako.
 
Umeandika makala ya kusifia uongozi ili kujikomba. Hiya haisaidii kabisa . Hawa tunawadai na mishahara yet
 
Amina..juwa hawa ni wahalifu na kwa Sheria walitakiwa wawe jela kifungo cha miaka 7

Kuwapa chochote kile ni kuhalalisha ajira yao

Hawa hawatapa chochote kile wamepoteza sifa za utumishi wao

Sijui kama kuna benefit yoyote ambayo watapata Nina Mashaka na hilo
 
Back
Top Bottom