Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Mkuu, shikamoo! Ukiwa kama moja ya wale niwapendao, sina budi kukupatia zawadi yangu kwa ajili ya mwaka mpya 2017. Sina pesa, sina mali lakini angalau Mwenyezi Mungu kanijaalia kuwa na mawazo ambayo yanaweza kuwa mazuri.
Mh. Rais, suala la kukosolewa “Critism” ni suala ambalo binadamu wote huwa hatulipendi. Hata hivyo, ni suala la kimaumbile kuwa; maadam mtu anaishi, anafanya vitu mbali mbali na anaongea na watu, ni lazima mtu huyo akosolewe tu. Ndio maana hata mwanafalsafa Aristotle katika moja ya maandishi yake akasema “Criticism is something we can avoid easily by saying nothing, doing nothing, and being nothing.” lakini kama mtu anatenda na anaongea, lazima atakosolewa tu, hayo ndio maumbile ya binadamu. Suala linalobakia nia amma apende au asipende kukosolewa lakini bado watu watakuwa wakikosoa ama kwa siri au dhahiri.
Mh. Rais wetu mpendwa; pamoja na kuwa kukosolewa daima kunakera; lakini kukosolewa ni kitu kizuri sana kwa anayekosolewa kuliko kwa anayekosoa kwani anayekosolewa huongeza maarifa lakini anayekosoa hakuna kipya anachojifunza.
Mh. Rais, mtu afanyapo jambo lolote lile; kupata mrejesho toka kwa jamii ni muhimu pengine kuliko kitu kingine chochote. Hebu jiulize kwa mfano unasema au unafanya kitu halafu jamii haitoi feed back!!? (au inatoa feedback ya kuigiza)!. Sasa feedback ndio inakuja kwa njia ya kushangiliwa, kukosolewa au kubaki kimya. Hata hivyo, wale wanaounga mkono, tayari wanakuwa washakubali kwa hiyo hamna wanachoweza kuongeza kwenye lile lililofanyika ili kuboresha na wanaokuwa kimya wanakuwa hawakotayari kuwajibika, bali wale wanaokosoa ndio wanaweza kuwa na maboresho.
Mh. Rais, Ukosoaji “Criticism” ni kama kioo. Ni vigumu sana mkuu, kwa mtu mwenyewe kujitathmini na kujua alivyo bali wale wanaomwangalia ndio wanaoweza kujua zaidi alivyo. Hii si kwangu au kwako tu mheshimiwa, lakini hebu kila mtu na ajiulize; ni mara ngapi ashawahi kufanya vitu akidhani yuko sahihi ila baada ya muda akabaini kuwa hayuko sahihi kutokana na “Criticism” za hadhira?. Pengine ndio maana mwandishi Frank A. Clark akasema “Criticism, like rain, should be gentle enough to nourish a man’s growth without destroying his roots.”
Mh. Rais, “Criticism” ni njia ya taarifa/ feedback pekee ambayo wanaoitoa huitoa kutoka kwenye nafsi zao bila unafiki. Kwa mantiki hiyo, inaweza kuwa ndio njia inayoweza kumpa mtu taarifa sahihi juu ya alivyo au alichokifanya kuliko njia nyingine yeyote.
Mh. Rais, “criticism” ni kitu kizuri kwa sababu humfanya mkosolewaji kudurusu yale anayoyafanya kila mara na kuona namna ya kufanya vizuri zaidi.
Mh. Rais wangu, mtu anayekosoa mwingine; haimaanishi kuwa anamchukia yule anayemkosoa bali anapenda afanye vizuri zaidi.
Kwa mantiki hiyo hapo juu, nakuomba Mh.Rais wangu mpendwa; wakati uingiapo mwaka 2017 uangalie kama ukiona inafaa na itakupendeza uwafanye wakosoaji wako kuwa “fans” wako na kutoka kwao, durusu yale wanayokueleza na chukua yale ambayo ni “constructive” na kuyafanyia kazi na utaona mrejesho wake utakavyokuwa wakupendeza kwa watu wengi.
Mh. Rais, hii ndio zawadi yangu kwako, nakuomba uipokee na kama utaipokea, naamini ni zawadi ambayo italeta matokeo makubwa sana kwenye uongozi wako na watanzania kwa ujumla kwenye mwaka 2017 na kuendelea.
Kwa heshma kubwa naomba kukukabidhi;-