Mh Rais Magufuli, nakuomba ubadilishe vile unaongoza sasa na ufungue ukurasa mpya

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,766
12,689
Mh Rais mim ni mmoja wa vijana nakupongeza kwa kaz nzuri umewafanyia watu wako na taifa kwa ujumla. Kwakweli hakuna mtu anaweza kubeza kaz yako nzuri umelifanyia taifa.

Mh Rais ata baada yakusema yote haya, mim kama mwananchi wa Taifa teule Tanzania ningependa uchukuwe muda wako kutafakari aina ya watu unawaongoza, maisha yao, tabia zao na ata mienendo yao ya maisha ya kila siku na ndipo umuombe Mungu jinsi ya kutoka nakuingia mbele yao. Nilazima ukumbuke kijiti ulichokabidhiwa na Rais mstaafu J. K kinasiri nzinto sana za taifa hili na kama Rais ukicheza vibaya ujuwe ni sawa nakuwasha kiberiti cha gas kwenye mapipa ya Petrol.

Mh Rais nilazima ukubali makosa yalitokea na njia pekee kuyatatuwa nikuwaita wazee wa taifa hili na watu wachama mkubaliane nini kifanyike. Watanzania walishazoeshwa aina fulani ya maisha kwa miaka kumi na wewe unakuja kuwaonyesha aina nyingine ya muongozo ambao hawaku uzowea kwa ten years. Katika hali kama hii nilazima Mh Rais uchukuwe tahadhari kubwa ili kuzuwia watu kukuona kama kiongozi usiwe wajali wala kuwathamini. Kumbuka mambo mazuri ya mtu huwa hayavumi kama ubaya mmoja ktk matendo elfu mema.

Mh Rais nilazima ukumbuke mtoto azaliwapo uwanza na maziwa ya mama kwa miez kadhaa mpaka kunywa uji na vitu vingine. Ukumbuke watu bado wanamambo mazuri waliyafurahia japo hayakuwa sawa ila ndivyo walizowea hivyo hawawezi toka kule kwa siku moja, nilazima kazi ifanyike.
Mh Rais nakuomba ubadilishe vile unaongoza sasa na ufungue ukurasa mpya wakuliongoza taifa hili kuelekea maendeleo ulituwahidi.

Jambo la kwanza kabisa kubali yapo makosa umeyagunduwa na kwa jinsi yeyote ile wewe kama Rais nilazima uyakubali maana serikali ilio pita ni ccm mliongoza na sasa ni ccm mnaongoza kwanini usiyakubali? Kumbuka kama uyakubali ilikuwa vyema kutokukubali nafasi ya uteuzi wa kuwa Rais ndani ya chama na kwakufanya hvyo ungeepusha madhara kwa chama na kwako pia kama Rais. Hivyo basi kama mh Rais umekubali kuwa Rais kubali ulio yakuta kutuokoa sote kama Taifa. Naiman umekubali.

Mh Rais kama umekubali jambo la pili yakupasa kufanya nikuchunga kile unakiongea mbele ya taifa. Bora kuwa bubu kuliko ongea maana wewe ni Rais unapo ongea neno watu wanalitafasiri kwa haraka sana hvyo bora ukiona unaongea na unahisi hasira itakuja basi soma hotuba ilio andikwa ili usiongee maneno yanaweza kulipua taifa. Mfano "Wazee ni wezi", Vilaza" nk. Kwakweli hayapaswi kutoka kinywani mwa Rais.

Jambo la tatu acha kupambana na watu tengeneza mfumo wakupambana na wa badhirifu maana usipo fanya hivyo utajikuta unazalisha majambaz badala ya majizi.

Mwisho kumbuka wewe Ni Rais wa jamuhuri umezungukwa na idara zote za usalama na upelelezi pamoja nakikosi hatari sana cha kumlinda Rais watumie hao kukuletea matunda chanya ktk kubadilisha mifumo mibovu ndani ya serikali kwakufanya hivyo watu watakuogopa zaidi pasipo kuwaambia nawarecord or which ever maana hakuna asie juwa hayo yanafanyika ila siri za taifa lazima uzichunge hata kwa kifo.

Mungu akutangulie Mh Rais.
 
Ukipitapita mtaani na baadhi ya vijiwe,utaona kuna baadhi ya watu muda wote ni kulalamika...mara oooh Raisi amezidi mno kutumbua majipu,mara oooh Raisi nchi imemshinda,ukimuuliza kwanini?anasema sukari imepanda bei....malalamiko yanaendelea mara ooooh Magufuli kamzalilisha Kikwete kwa kumuambia serkali iliyopita imemwachia mzigo mkubwa,maana anapogusa "hewa".najiuliza maswali hivi wapinzani wamepata nguvu wapi ya kumpongeza kikwete kwamba alikuwa kiongozi bora?hawa ni wanafiki hupenda kukuza hata jambo dogo....Wapinzani wa Tanzania wamekuwa watu wa matukio...Ishu ya wanafunzi UDOM nalo wamelikomalia sana....imefikia hatua wanamrusha mtoto wa Raisi mitandaoni kwamba mbona aliferi form four afu yuko chuo kikuu?ni maneno ya wakosaji....RAISI UKO SAWA SISI TUNAKUUNGA KWA DHATI MKONO.
 
Machadema ndio yanaharibu nchi kwa kisingizio cha demokrasia.

1. Yalisema lowasa fisadi Leo ndio yaosha miguu yake

3. Yalisema katiba ni mbovu ,lkn sasa yanaandaa maandamano nchi nzima kutaka katiba ifuatwe.

Majitu mazima na ndevu lkn kazi kulialia tu kila siku
 
Back
Top Bottom