EWGM's
JF-Expert Member
- Jul 22, 2013
- 1,521
- 2,112
Mheshimiwa sana Mwigulu Nchemba nikupongeze kwanza kwa kuchua hatua ya haraka ndani ya masaa 24 na kumuagiza IGP amshughulikie yule muhuni wa jana aliyemtolea Mheshimiwa Nape Nnauye bastola. Nadhani sasa ni wakati muafaka wa kulichukulia jambo lile kama changamoto na kufanya maamuzi ya kihistoria ambayo yataingiza jina lako liandikwe kwa wino wa dhahabu kwenye vitabu vya kumbukumbu ya nchi hii.
Mheshimiwa, waungwana wanasema kila kwenye baya kuna mazuri hujitokeza, na sasa nafikiri ni wakati wa kutwaa mfumo wa shirika la anga kwa kutumia “Black Box Thinking” katika shughui zetu za kila siku. Badala ya kuchukua hatua kwa jambo linapotokea tuwe tunafanya maamuzi ambayo yatakuwa endelevu na ya muda mrefu ili kuzuia majanga mengine makubwa zaidi kama hayo yanayoweza kutokea kwenye siku za usoni.
Mheshimiwa sana naona sasa ni wakati muafaka kwa Tanzania kuwa na Tume Huru (Tanzania Independent Police Complaints Commission, TIPCC) ya Kudumu ya kupokea na kufanyia kazi Mamalamiko yote yanayohusu Jeshi la Polisi. Tume hii iundiwe kisheria na iwekwe kwenye Police Act za nchi hii na ipewe nguvu na mamlaka ya kushughulikia wahuni wote wanaotumia magwanda na ngao ya Taifa kutimiza mauovu yao bila kuingiliwa na upande wowote.
Kwa kuwa hili ni jambo la kitaifa kaeni pamoja na Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Godbless J Lema pelekni muswada Bungeni ili kukomesha udhalimu huu wa mahuni wachache waliojipenyeza kwenye Jeshi la Polisi ili kuwalazimisha na kulifanya jeshi letu la Polisi kuwajibika kutokana na viapo walivyokula kabla na baada ya kuvaa na maganda na kuibeba ngao ya nchi.
Tume hii isimuhusishe Raisi wala serikali katika kuchagua Mwenyekiti na makamishna wake na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lihusike moja moja kupitia kamati zake za maadili na uadilifu katika kuwahoji na kuwachuja wale wote watakao omba nafasi mbalimbali kwenye Tume hii. Bunge liwe na mamlaka ya kutengeua na kumwajibisha kiongozi wowote wa tume hii itakapobainika hayuko sawa na mlengwa mzima wa tume hii.
Mheshimiwa, Jeshi letu la Polisi limekuwa likifanya mateso na unyanyasaji mkubwa kwa raia wa nchi hii kwa muda mrefu sana sasa. Jeshi la Polisi limeshahu kabisa wajibu wake wa kulinda sheria za nchi ili wananchi wazifate na kusisitiza ustaarabu kwa jamii. Lakini ikiwa Jeshi lenyewe linakosa ustaarabu na kuanza kufanya vitendo vya kihuni kwa raia wake nadhani wewe kama Waziri kijana mwenye dhamana na Jeshi hili una wajibu mkubwa wa kuweka mambo sawa.
Niseme kwa uwazi tu Mheshimiwa, kilichotokea jana hakikunistua sana kwasababu mambo kama hayo huku mtaani tumeyazoea na pia ni yakawaida kwetu kwa kila siku ijapokuwa si sahihi. Ila tushukuru na pia ni heri kuwa limeweza kutokea kwa Mheshimiwa Nape na kuweka msisitizo wa mabadiliko kwenye nchi yetu ili watoto wetu waishi maisha kwa amani kama inavyopaswa bila ya kuwa na woga kwa pande zote mbili; Jeshi la Polisi na Makundi ya Wahalifu.