Naelewa machungu yako, lakini hayabadilishi ukweli kwamba Mamlaka iliyopo imechaguliwa na Watanzania kwa wingi wao, wenye maji na wasio na maji, wenye umeme na wasio na umeme, Maskini na Matajiri hivyo wote kwa ujumla wetu hatuna budi kuitii, ndio demokrasia yenyewe hiyo, na kama tunaona haitutendei haki tuna uwezo wa kuibadilisha 2015 na kuweka Mamlaka ambayo itafanya yale yanayotupendeza, ila kwa sasa hatuna jinsi!
Isitoshe hata Wapinzani nao siku moja watapewa Mamlaka ya kuongoza na Watz, ninaweza kukuhakishia sio 100% yetu tutawachagua, lkn kwa kuwa wengi watakuwa wamewachagua wengine tuliobaki tutakuwa hatuna budi pia kutii Mamlaka watakayokuwa nayo, sasa kama kila mtu akisema kwa kuwa hapendezwi na maamuzi ya Mamlaka iliyochaguliwa kihalali aandame hata kama Mamlaka imemkataza, pia wao watashindwa kuongoza, na watatumia njia zilezile ambazo Mamlaka ya sasa hivi inatumia, hakuna jipya Dunia hii tumeona Afrika Kusini, ANC wanatumia jeshi lile lile na mbinu zile zile kuuwa watu walewale waliokuwa wanawapigania miaka yote!
Demokrasia ni ngumu sana!