Mh Kigwangala asipuuzwe

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,289
Reaction score
2,472
Nimeikuta Facebook na kwa ridhaa ya mhusika kanikubalia kuiweka humu
...................................................................................
Kwa kilichotokea hapo majuzi kwenye usaili wa watakaokuwa wafanyakazi wapya wa TRA ni muendelezo tu wa mazoea yetu kama watafutaji. TRA ilipokea maombi 56,000 kwa nafasi 400 za ajira lakini kwa mujibu wa vyanzo kadhaa [Malisa G.J -fb] waliofika ni 30,000. Lakini hilo pia halitoshi kuhalalisha uwepo wa idadi hiyo kubwa. Inaonesha kuna tatizo kubwa kwa pande zote zinazohusika.

Kwanza serikali ambayo kazi yake kubwa wala si kuajiri bali kuweka miundombinu rafiki kwa wananchi wake katika kufikia mahitaji muhimu. Hii miundombinu ni pamoja na mawasiliano [barabara, madaraja, majini, angani, upatikanaji wa habari, gharama nafuu za kupata haya mawasiliano], upatikanaji wa huduma [maji, umeme, masoko, huduma za afya], na kuhakikisha uchumi wa nchi angalau unakuwa imara. Pamoja na kuweka sera zinazotekelezeka hasa linapokuja suala la ubunifu. Wako vijana wengi wana vipaji na taaluma za ubunifu lakini hawafiki popote. Wakiwa na ujuzi wa kupitiliza wanaishia kuibiwa na mataifa yanayojua thamani ya rasilimali watu. Hayo ni kwa uchache.

Taasisi za kielimu nazo kwa upande wake zina wajibu wa kuona kuwa wanatoa elimu ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na wakati tunaoishi na wakati ujao kutokana na kupata picha ya mbeleni. Elimu zisiwe za kinadharia sana na wala wanaosoma wasipewe matumaini sana kuwa ukimaliza ajira ni nje nje. Hata kama ni nje nje waambiwe ni ajira za aina gani ziko nje nje maana wengi wanafikiri ajira ni kuajiriwa tu.

Sasa tukija kwa wahitimu wenyewe, pamoja na kupeleka lawama kwa serikali [kitu ambacho ni kweli] kuna suala la kupambana na hali ya mhusika. Ajira ni changamoto kweli lakini kama alivyosema Dr Kigwangala kuna ukweli kuwa vijana ndani ya wimbi hili la ufinyu wa ajira, wanachagua kazi. Utajiuliza kama waliomba elfu 56 na wakaenda elfu 30 ni wazi kuwa hao ambao hawakwenda wana ajira zao. Hata hao waliohudhuria pia yawezekana nusu na zaidi wana ajira ya aina moja au nyingine.

Tujiulize pia kuwa ajira hiyo wangetangaza taasisi nyingine isiyo na ukwasi kama TRA ni kweli wangeenda wote hao? Kuna suala la 'greener pasture'. Yani malisho ya kijani. Yani kusaka kipato bora zaidi. Hiyo ni hulka ya binadamu. Ifike mahali vijana waanze kujiamini katika yale wanayofanya. Kusubiri watu/taasisi zijijenge halafu mtu abebe vyeti kuanza kuomba kazi hilo ni tatizo.

Kuna kitu tumejijengea akilini hasa wale wahitimu wa shahada, kwamba kazi fulani ni za kina fulani. Na hizi ni za kwetu. Hizo zama kwa sasa zinapitwa na wakati. Katika zama hizi za teknolojia mtu yoyote anaweza fanya lolote kama akiamua [ukiondoa taaluma chache zinazohitaji kweli kusomea mambo hayo]. Suala la kutafuta pesa halifungamani na taaluma ya mtu. Ujasiriamali na biashara si mambo yaliyojaliwa watu wachache. Mtu yoyoye anaweza kuwa mjasiriamali au mfanyabiashara.

Wanasema INFORMATION IS POWER. Hawakukosea waliposema hivi. Tatizo watu wengi hatupendi kuamini kilichoandikwa au kinachosemwa na watangulizi, ambao tunawaita wahenga. Kuwa na taarifa nyingi za masuala mengi kutakupa uhuru wa kifikra. Uhuru wa kuamua na kuchagua. Si lazima tukae maofisini. Ofisi za watu na kungoja mishahara. Itafika wakati huu mfumo wa Kizamani [traditional] kuajiriwa utakoma. Ajira zitakuwa katika mifumo tofauti sana.

Information is power. Cha msingi ni vijana kuandaliwa na wazazi na walezi wao kuwa mawazo mbadala. Ubunifu si lazima kubuni simu. Ubunifu ni pamoja na kuongeza thamani za vile vilivyopo, kama karanga za Diamond. Tufikirie na wala tusiwe na ukomo wa kufikiri, hata ikibidi kufikiri #nje_ya_box kama alivyofanya Mh. Waziri
 
Wapoti Mh. Kigwangala hajakosea kabisa, na hata unachosema wewe ni kweli, kwa kweli ile vurumai tuliyoiona pale ni AIBU..
Yaonyesha hata watu HR wa @TRA walio na degree mpaka Masters wako disorganised! Ila tunashangaa kivipi mkuu?! Ndiyo kawaida yetu, umeshuhudia tu juzi kule London Kamanda Alphonce Simbu kushinda Bronze, hakuna cha kupewa bendera wala nini! Umeshuhudia Customer Services kwenye taasisi, mashirika na wizara kulivyo shaghala baghala! Jinsi wanavyowaona wateja kama uchafu! Haijalishi kwao kama wawapelekea biashara au hela! Walivyoomba kazi wengi wao walitoa rushwa za kila aina na kuswali kupita kiasi waipate hiyo kazi, walivyoipata wamesahau kabisa majukumu yao pale..
Kidogo sana twajirekebisha, ndiyo maana wengine wanawapenda Wakenya, mtaani au wakati wa kufunguwa ofisi hakuna salaamu, ila ukiingia ofisini kwake kibiashara unapokewa kama Mfalme kama sio Malkia! Ila twajifunza?! Sidhani...
 
Kama Hujui Ni Hvi Wale Elfu 30 Ndio Walioitwa Kwenye Interview Na Waliobaki Hawakukizi Vigezo Vya Kufanyiwa Interview Sio Kwamba Wanakaz Nyingine
 
Kama Hujui Ni Hvi Wale Elfu 30 Ndio Walioitwa Kwenye Interview Na Waliobaki Hawakukizi Vigezo Vya Kufanyiwa Interview Sio Kwamba Wanakaz Nyingine
Nami nimeiweka tu hapa kama nilivyoipokea, mkuu. Ila uko sahihi
 
Matokeo yake wenye mamlaka wanaanza kuzodoana. Kigwangala alitaka kupunguza makali ya kile kilichotikea kwa kuamini kuwa si wote hawana ajira. Wenzie akiwemo Mbunge wa Chalinze na mkuu wa mkoa wa Simiyu wakimshukia kama mwewe. All in all hili halikupaswa kutokea au kuonyeshwa kwa maana ni aibu na udhaifu kwa serikali
 
Ajira tatizo ni si kwamba watu wanapenda kupata ajira TRA.......wenye kazi zaohawafiki asilmia 10 hapo........
 
Ni kweli ila pia kumbukeni Hakuna Nchi yoyote ile Duniani yenye Ajira za kuwatosheleza Raia wake! Vijana tuwe wabunifu
 
Tatizo la nchi yetu ni mtu kuamka usingizini na kuchukua Trilioni 1 eti akajenge uwanja wa ndege nyumbani kwake.

Mtu achukue Trilioni 2 eti akanunue Bombadier? Watanzania wangapi wanatumia usafiri wa anga ukilinganisha na wabarabara na uwiano wa watu takribani milioni 50!!

Je kipaumbele ni Ndege?

Africa, hasa Tz tatizo kubwa ni vipaumbele na shida nyingine ni kutambua changamoto zipi zipewe kipaumbele.

Badala ya mtu kuchua Trillioni 3 kuweka ktk Kilimo vijana tukalime. Yy na ndege tu. Hashauriki.

Sekta binafsi yote nchini ipo hoi. Huyu ndie muajiri mkuu nchini. Yy anafurahi "na mtakufa tu hakuna hela bure" utadhani alisha wahi kumlisha mtu.

JPM KAMATA WEZI
 
Tulidhani angekuwa na mtazamo huo ila imekuwa tofauti. Matokeo yake ajira zilisitishwa ili ipatikane hela ya kujikimu wao
 
Ni kweli ila pia kumbukeni Hakuna Nchi yoyote ile Duniani yenye Ajira za kuwatosheleza Raia wake! Vijana tuwe wabunifu
Cha msingi sisi vijana yatupasa kufanya kazi ya aina yoyote yenye kukidhi mahitaji yetu ya kila siku tuache kutegea kitu au kazi fulani tuliyojiaminisha kua ndiyo kazi ambayo inafaa kwetu.
 

Ukweli ni kwamba hao HRM wa TRA hawajuwi wanchofanya. Hakuna sababu ya kuita watu maelfu kwasaili. Unapitia barua zote za maombi unategeza short list ya wale wanaokidhi mahitaji ya post, kisha unawapelekea nauli ya kuja na kirudi na par diem hao wachache. Waliobaki unawaarifu kwamba hawakifanikiwa. Utaratibu huu unakidhi dhana ya equal opportunity in employment. Vinginevyo watoto wa mikoani hawatakuwa na uwezo wa kujilipia nauli na malazi labda wale wa wazazi matajiri.
 
Ndugu si kwamba watu wanachagua kazi...saivi ajira ni shuguli pevu ndugu yangu...toka magu aingie makampuni kibao yamepunguza idadi ya wafanyakazi..bado pia kuna mlundikano mkubwa Wa vijana wasio na ajira mtaani...pia katika ishu ya kujiajiri jaribu kuangaliana mfumo wa elimu yetu...!! Watu waliopo juu daima haoni huku chini that's so kigwangala kujifanya anashangaa ni kujifanya kipofu wakati anajua hali halisi...mnafiki nae

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hivyo kujifanya wanajua fair play
 
Ndio maana nami nikasema kuwa si jambo la mara moja. Vijana wajiandae na waandaliwe. Ni mchakato. Ifike wakati kijana ajue hakuna kazi ya machinga au msomi. Ni yeye kwa jinsi gani anaiongeza thamani hiyo kazi kutokana na elimu yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…