Fandre
JF-Expert Member
- Sep 20, 2013
- 320
- 225
Mh. Hussein Bashe ambaye wengi wamekuwa wakimuita kama KIBOKO YA KIGWANGWALA ndiye Mbunge tokea Chama Cha Mapinduzi anayeonekan kuwa ndiye atakuwa mwenye uwezo wa kujenga hoja za nguvu na kuisimamia serikali kikamilifu kama katiba na kanuni za bunge zinavyosema.
Akiwa tayari ameshaweza kutoa maonyo makali kwa viongozi waandamizi wa Chama cha Mapinduzi kama lile alilompa mwanadiplomasia mkubwa nchini Mh. Bernard Membe kuhusiana na kukaa mbali na kumuacha Mheshimiwa Magufuri afanye kazi tayari ameendeleza makali yake na sasa ameamua kwa dhati kupambana na masuala ya ufisadi unaoangamiza sana taifa hili kwa muda mrefu.
Mheshimiwa Bashe amesema, tatizo kubwa linalosababisha taifa hili kuangamia ni kuwepo kwa sheria nyingi zinazoruhusu wizi, ukwapuaji na kila aina ya ufisadi ni uwepo wa sheria ambazo zilitungwa makusudi na wanasiasa ili baadae waweze kula kiulaini mali za taifa hili pamoja na fedha za walipa kodi wa nchi hii.
Mheshimwa Bashe pia, amemtaka Mheshimwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Sospeter Muhongo kuhakikisha makubaliano na mikataba yote17 iliyosainiwa kwa siku moja inarudishwa bungeni ili iweze kutumbuliwa majipu yaliyomo ndani yake.
Mheshimwa Bashe, hakuishia hapo bali pia aliwaambia wabunge wa vyama vya upinzani wasiwe wanapinga kila jambo kwani kuna baadhi ya mambo ni ya haraka na yanahitaji ufumbuzi wa haraka, huku akitolea mfano maamuzi ya Magufuri kuruhusu utolewaji wa Fedha za ujenzi wa barabara ya Mwenge hadi Morocco.
Mheshimiwa Bashe anatajwa kuwa kiongozi makini na kijana mwenye muono mkubwa ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi, huku akionekan kuwa miongoni mwa vijana wachache ndani ya chama hicho ambao wana uwezo mkubwa wa kubadili taswira ya chama na kukifanya chama chenye nguvu ya ushawishi na ushindani mbele ya watanzania.