Mh Ghasia : Tunaomba Utekeleze Ahadi zako na Pia Ilani Ya CCM

SEBM

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
495
325
Jana (08/05/2012) katika taarifa ya habari ya saa mbili usiku kupitia ITV, mtangazaji Renatus Mubabuzi aliripoti juu ya kuharibika kwa mkokoteni uliokuwa unatumiwa na wananchi wa Kiromba/Nanyamba, Wilaya na Jimbo la Mtwara Vijijini kwa ajili ya kuwabebea wagonjwa na kuwapeleka katika vituo vikubwa vya afya.

Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo aliiomba serikali iwasaidie gari la kubebea wagonjwa, lakini hata Pikipiki ingewafaa tu.Habari zilipasha kuwa mkokoteni ule ulioharibika, ulikuwa unategemewa na vijiji vipatavyo vinane.
Mh. Hawa Ghasia, tunakuomba utekeleze ahadi zako na pia ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ( 66(j))
 
Kaka mm nimeona hyo story ni aibu kwa karne hii kwa kweli tafadharini wabunge wa mkoa wa mtwara unganeni kuondoa aibu hii ombeni hata mashirika ya dini au ngo,s zisaidie hii ni balaa
 
Nyie wananchi wa Mtwara kwann mnawachagua hao magamba miaka yote ss hiyo ndio shukrani yao. Karibu kwe2 tumehamasika na kuhamia M4C na ukombozi utaendelea ili kuuharakisha ufike kwenu vueni kwanza hayo magamba
 
Back
Top Bottom