Mgosi: Wachezaji wa Simba Tunastahili Kuuawa

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Mshambuliaji mkongwe na nahodha wa kikosi cha Simba SC Musa Hassan ‘Mgosi’ ameshindwa kujizuia kuonesha kusikitishwa na matokeo mabaya ya klabu yake katika siku za hivi karibuni na kufikia kusema wachezaji wote wa Simba ndiyo wanastahili kubeba lawama za matokeo hayo na si mtu mwingine yeyote.

Mgosi hakuishia hapo akaenda mbali zaidi na kusema anadhani wachezaji wa Simba wanastahili kuuawa wote kwasababu hawaitendei haki timu yao. Inasikittisha sana, kwa mtu mwenye akili timamu na anayejua Simba inataka nini, lazima aumie. Nafikiri kama ingekuwa kwenye nchi nyingine basi ningeruhusu wachezaji wote tuuawe kwasababu hatuitendei haki Simba. “Kila siku tumekuwa tukisema wenzetu wanapendelewa, sisi tunapata nafasi tunashindwa kuzitumia mwisho wa siku lazima lawama tukubali sisi.

Mechi ambazo ni muhimu kwetu tunashindwa kucheza, hakuna kulaumu kiongozi, kocha wala mtu mwingine yeyote, kwasababu wao wanatimiza majukumu yao wanapeleka timu kambini, watu wanakula, mishahara wanapata, tukishinda bonus inatolewa sasa hapo kiongozi analaumiwa vipi?”, anahoji Mgosi ambaye alipata mafaniko na simba katika miaka ya 2005 hadi 2011. “Lawama zote tupokee sisi wachezaji ndiyo tunasababisha Simba iwe hivi”, alimaliza nyota huyo aliyetamba na Mtibwa katika misimu ya 2013-14 na 2014-15 kabla ya kurejea tena Msimbazi msimu huu.
 
Laana ya Mafisango.. Sahau ubingwa tena Bara.
Mgosi bwana!!! Aliaminiwa kule Manungu yeye akakimbilia Matopeni, Sasa hivi anataka wachezaji wote wale Panga la shingo duuuuu!?!!!!!
 
Wauweni tu wachezaji wenu sisi wetu wako kimataifa zaidi
Kessy huyooooooo Jangwani kwa Miaka miwili, Alijua kuna siku kule Matopeni watauana tu akaona isiwe taabu bora awaache wauane wenyewe.
Hongera kessy Karibu Jangwani upande Ndege Deileeeeeeeee, huku hakuna habari ya Kupanda Ngalawa kama kule Manyoyani fc
 
Naona mgosi anajitahidi kuJipendekeza kwa mabosi wake kwa kuwakandia wenzake eti wachezaji wote wauliwe utafikiri yeye kama huwa hache vile tena mbaya zaidi hata hata kagoli ka offside kwenye ligi kuu
 
Mshambuliaji mkongwe na nahodha wa kikosi cha Simba SC Musa Hassan ‘Mgosi’ ameshindwa kujizuia kuonesha kusikitishwa na matokeo mabaya ya klabu yake katika siku za hivi karibuni na kufikia kusema wachezaji wote wa Simba ndiyo wanastahili kubeba lawama za matokeo hayo na si mtu mwingine yeyote.

Mgosi hakuishia hapo akaenda mbali zaidi na kusema anadhani wachezaji wa Simba wanastahili kuuawa wote kwasababu hawaitendei haki timu yao. Inasikittisha sana, kwa mtu mwenye akili timamu na anayejua Simba inataka nini, lazima aumie. Nafikiri kama ingekuwa kwenye nchi nyingine basi ningeruhusu wachezaji wote tuuawe kwasababu hatuitendei haki Simba. “Kila siku tumekuwa tukisema wenzetu wanapendelewa, sisi tunapata nafasi tunashindwa kuzitumia mwisho wa siku lazima lawama tukubali sisi.

Mechi ambazo ni muhimu kwetu tunashindwa kucheza, hakuna kulaumu kiongozi, kocha wala mtu mwingine yeyote, kwasababu wao wanatimiza majukumu yao wanapeleka timu kambini, watu wanakula, mishahara wanapata, tukishinda bonus inatolewa sasa hapo kiongozi analaumiwa vipi?”, anahoji Mgosi ambaye alipata mafaniko na simba katika miaka ya 2005 hadi 2011. “Lawama zote tupokee sisi wachezaji ndiyo tunasababisha Simba iwe hivi”, alimaliza nyota huyo aliyetamba na Mtibwa katika misimu ya 2013-14 na 2014-15 kabla ya kurejea tena Msimbazi msimu huu.

Hata yeye nae ATUPISHE tu kwani wenzake walikuwa wakifanya mazoezi ya mpira yeye kutwa alikuwa anafanya kazi ya kumpa tu UJAUZITO mkewe.
 
Haaaaaa haaaaaaaa mkuu GENTAMYCINE unaonekana una hasira sana na Viongozi wa Simba!!!!!
Nasikia wachezaji 7 wa kigeni wamegoma kuondoka leo kuelekea Songea kwa ajili ya mpambano dhidi ya Maji Maji.
 
Karibuni Songea Simba.
Mtachokipata itakua siri yenu.
Tafadhali wanalizombe msiwafunge hao mikia watazidi kushikwa na hasira wakauana bure!!!!! Badala ya kuwa timu ya mpira wa miguu itageuka kuwa Al shabab
 
Simba hii inahitaji msasa wa hali ya juu, sioni hata first 11 hapo ya kuchukua ubingwa. Timu hii yote ni squad players, na uongozi wa wale MAFIOSO kamwe hatutashinda ligi wala kupanda ndege.
 
baraaaaaaaaa.........
Tena hilo balaaaaaa sio la kitoto, wakati Mgosi akitamka hayo huku kunaibuka lingine la wachezaji wa kigeni wa timu hiyo wamegoma kuondoka na timu leo kuelekea Songea kupambana na Maji maji. Hii Simba hii.......
 
Yeye mwenyewe licha ya huo u captain hakustahili kuwa mchezaji wa simba kama watu makini wapo.Tatizo la mifumo ya hizi timu zetu ni khatari kwa afya ya timu pana watu wana mamlaka makubwa sana na ndio wameshika mpini.Hizi timu bila kuwa na uongozi madhubuti na vyanzo endelevu vya mapato kila mwaka zitakuwa zinatuongezea wagonjwa wa presha.
 
Eti unamtoa Hamis Kiiza halafu unategemea Mgosi akabadilishe matokeo!!!? Utani huu
 
Michael Wambura alikuwa mtu wa Mpira lakini kwenye ule uchaguzi aliundiwa zengwe balaa,tukae chini wana simba tusuke kikosi chetu upya niliwahi kusema wachezaji wetu utoto mwingi.
 
Back
Top Bottom