Mgomo wa wafanyakazi wa Kampuni ya sukari Kilombero

Mwinjilist mtume nabii

JF-Expert Member
Feb 21, 2015
2,437
1,098
Kufuatia kikao cha wafanyakazi kilichofanyika tarehe 17/6/016, makubaliano yaliyofikiwa ni kwamba wafanyakazi wamekataa kufanya Massa ya ziada hvyo baada ya kutimiza masaa ya kawaida ya wiki ambayo ni 45 mpaka Jumamosi saa 5 asubuh, wataondoka kwenda nyumbn mpk Jumatatu ivyo na kuwaachia mameneja na wazungu wafanye wenyewe.

Mgomo huo unakuja baada ya mvutano wa muda mrefu kati ya Mwajiri na chama cha wafanyakazi TPAWU ambapo mwajiri alianza na nyongeza ya 2% na chama kilitaka 20% toka mwezi 3.

Mpka sasa mwajiri ameishia 6% huku chama kikihtj angalau 11% baada ya kikao cha mwisho kilichofanyika tar 7 June kilichoudhuriwa pia na wakuu wa wilaya ya Kilosa na Kilombero kwa agizo LA Waziri kwmb wawepo.

Ingawa kwny kikao imeonekana wakuu hao wa wilaya kuwa upande wa mwajiri kwa SBB chama kilionana na Mbunge Wa Mikumi Profesa Jay ambaye aliwaunganisha na mawaziri watatu, wa Viwanda, wa Kazi, na waziri wa Kilomo.

Kitendo hicho kimeonekana kuwakera wakuu hao wa wilaya na hata kumwita m/kiti wa chama icho cha wanyakazi Ndg Isaack Magasa kumuhoji.

Lakini wafanyakazi wanataka mambo makuu mawili ambayo ni:
1. Nyongeza ya 11%
2. Kujiuzuru kwa meneja uajiri Ndg Beda Chacha Marwa ambaye amekuwa ndo chanzo cha matatzo hao kwan inasemekana wazungu wapo tayari kulipa iyo lkn huyu ambaye ni Mtanzania ndiye kikwazo kikubwa.

Hivyo wafanyakazi watakaokuwa zamu kesho asub uh wanakumbushwa kutoka Kzn saa5 km ilivyokubaliwa na atakaebaki kazini asiwalaumu wenzake watakachomfanya.
 
Back
Top Bottom