Mgomo wa madereva unachochewa na UKAWA

Mgomo wa madereva unachochewa na UKAWA

mzee wa liver

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
83,468
Reaction score
431,954
Mh Waziri wa Kazi amemaliza kutoa mchango wake Bungeni na kusema mgogoro wa madereva na Serikali unasababishwa na kuchochewa na Mbunge mmoja wa upinzani anayetoka Mkoa DSM kwa sababu amekuwa akiwapigia viongozi wa umoja wa madereva na kuwaambia nini cha kufanya wana JF mnasemaje kuhusu hili kuna ukweli ndani yake.
 
...kama unachochewa na ukawa au mbunge wa dar, hii sio ishu cha msingi ni je, madereva wanaishu za msingi..? serikali imefanya nini..? imetimiza wajibu wake..? kisha njoo utafute mchawi. kama madereva wana hoja za msingi basi anaye chochea mgomo wa madereva ni serikali kwa kutotimiza wajibu wake na waache kusingizia wengine....
 
Hivi ni visa vya mbaazi.

Ni vizuri huyo waziri akajaribu kupanua wigo wa ubongo wake. Asidhani kwamba kwa kuwa ccm imewekeza katika ujinga basi watanzania wataendelea kuwa majuha wasijitambue siku zote.

Madreva wametoa malalamiko yao, serikali imeyasikiliza na hatimaye mara mbili kutamka kwamba ni madai halali na serikali imeona kuna hoja za kushughulikia. Huo uchochezi leo umetoka wapi?

Kwamba wamechochewa kujua haki zao au wamechochewa kutambua kwamba maisha yao yanashida na wanazidi kuumizwa?

Hainiingii akilini kwamb atuna mawaziri wa kiwango kile.

Mtu akiwa anaumwa kichwa, maumivu makali hadi anatoa machozi, kuna hitaji mtu wa kumchochea ili ajue kichwa chake kinamuuma? Machozi yanapomtoka kwa maumivu, utakuwa na akili timamu ukiacha kumtafutia tiba kama unamjali, au kuanza kutafuta nani kamwambia atoe machozi? Kwamba kulia machozi ya maumivu hadi kuwepo mchochezi?

Huu sasa ni zaidi ya wendawazimu!.

Madreva, waoneni hao mawaziri wa ccm walivyo na nia ovu, ufahamu mdogo huku wamejaa hila. Juzi walisema kinafiki kwamba shida zenu ni za kweli. Leo wamekaa kimya hawataki kutafuta suluhu, wanatafuta nani aliyewaambia mseme mnaumia!. Ni dharau iliyoje? Kwa mtaji huo, ni dhahiri Chama Cha Mapinduzi, kimewafanya Watanzania matutuso wasiojitambua hata wangeumizwaje, wabaki wakicheka cheka na kupiga makofi ya ahsante. Na kwamba hawatakiwi kujitambua na kujitambua ama kueleza maumivu ni sawa na msukule kaasi kambi, anatafutwa aliyemzindua!.

KUNA SABABU GANI JAMANI YA KUENDELEA KUONGELEA SERIKALI YA CCM? WATANZANIA AMKENI. CCM INATAKIWA IONDOLEWE OCTOBER, VINGINEVYO MTAKUWA MISUKULE ISYOTAKIWA KUTUMIA AKILI NINYI NA WATOTO WENU WOTE!.

Waziri amaeudhi.
 
Huyo ndio waziri na huo ndio uwezo wake wa kufikiri na ni waziri huyuhuyu alishasema kuwa suala la madereva kusoma wakati wa kurenew leseni si la serikali bali yule kiongozi wa NIT alilitoa tu mwenyewe.
 
Mh Waziri wa Kazi amemaliza kutoa mchango wake Bungeni na kusema mgogoro wa madereva na Serikali unasababishwa na kuchochewa na Mbunge mmoja wa upinzani anayetoka Mkoa DSM kwa sababu amekuwa akiwapigia viongozi wa umoja wa madereva na kuwaambia nini cha kufanya wana JF mnasemaje kuhusu hili kuna ukweli ndani yake.

Nikikumbuka ule wimbo wa Tundu Lissu kule Bungeni sipati shida kabisa! Hivi kwa akili ya kawaida tu huyo mbunge wa UKAWA kutoka DSM ndiyo anaongoza Serikali!? Kama ndiyo hivyo basi huyo Mbunge ndiye wa kumsikiliza kwakuwa ananguvu ya ushawishi wa kuiwajibisha Serikali! Hiyo haiondoi ukweli kuwa "Serikali ya CCM imechoka!"
 
kunyoosheana vidole siku zote ni kushindwa uwezo wakufikiri!!! tunaitaji viongozi wanaotatua matatizo!!!
 
Mh Waziri wa Kazi amemaliza kutoa mchango wake Bungeni na kusema mgogoro wa madereva na Serikali unasababishwa na kuchochewa na Mbunge mmoja wa upinzani anayetoka Mkoa DSM kwa sababu amekuwa akiwapigia viongozi wa umoja wa madereva na kuwaambia nini cha kufanya wana JF mnasemaje kuhusu hili kuna ukweli ndani yake.

Ni kweli?// kama ni kweli sio hilo bali haya yafuatayo.

  1. Mafuriko ya Dsm ni kazi ya ukawa.
  2. Kushuka kwa thamani ya Shilingi kazi ya ukawa.
  3. Ufisadi ni kazi ya ukawa.
  4. Ajali za barabarani kazi ya Ukawa.
  5. Kudorora kwa huduma za afya hospitalini ni kazi ya Ukawa.
  6. Kudorora kwa uchumi wa nchi ni kazi ya Ukawa.
  7. Uchache wa BVR machines ni kazi ya Ukawa........................................................................................................................Ni akili au matope?
 
kunyoosheana vidole siku zote ni kushindwa uwezo wakufikiri!!! tunaitaji viongozi wanaotatua matatizo!!!

ni kweli dino waziri ajatatua tatizo la msingi la madereva tutarajie migomo mingi mbele yetu
 
Ni kweli?// kama ni kweli sio hilo bali haya yafuatayo.

  1. Mafuriko ya Dsm ni kazi ya ukawa.
  2. Kushuka kwa thamani ya Shilingi kazi ya ukawa.
  3. Ufisadi ni kazi ya ukawa.
  4. Ajali za barabarani kazi ya Ukawa.
  5. Kudorora kwa huduma za afya hospitalini ni kazi ya Ukawa.
  6. Kudorora kwa uchumi wa nchi ni kazi ya Ukawa.
  7. Uchache wa BVR machines ni kazi ya Ukawa........................................................................................................................Ni akili au matope?

Faiza Foxy na Juliana Shonza mko wapi mje mjibu hili swali!
 
Eti imeundwa tume,tumeona tume ngapi tz hii na hakuna jipya?tena nyingine zimeundwa kwenye vyumba vya ikulu na hakuna lolote itakua hii ya dc checkibob?
 
lakini ukiangalia kwa undani hivi ni mbunge gani wa upinzani aliyesema madereva wakasome kila baada ya miaka mitatu ni mbunge gani wa upinzani aliyesema madereva hawana mikataba mizuri ni mbunge gani wa upinzani aliyesema ratiba ya sumatra na polisi zinapishana ni mbunge gani wa upinzani aliyesema matrafic wanasumbua barabarani so waziri wetu wa kazi na ajira tunaweza kusema amekurupuka kwenye majibu yake kwa sababu bado hajibu kero za madereva na nina wasiwasi kesho kutwa ukasikia mgomo mwingine kwa kukwerwa na majibu dhaifu ya waziri
 
Na mimi naombea utokee mgomo mwingine wa Madereva wote wa vyombo vya usafiri wa umma ili Watanzania wapate akili maana ni wepesi wa kurubunika na kusahau! Hadi CCM na Serikali yake watie akili, wakumbuke wajibu wao maana wamejisahau sana! Lakini nasikitika muda wa kuwashauri haupo umekwisha maana kama wameshindwa miaka zaidi ya 50 kujirekebisha, wataweza kutekeleza miezi 3 iliyosalia!? Labda kwa miujiza!!!
 
Back
Top Bottom