Mgomo wa madaktari: Napingana na askofu Kilaini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari: Napingana na askofu Kilaini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Plato, Feb 9, 2012.

 1. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #1
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  Mwandishi wa maneno haya ni mkatoliki anayejua uzito wa kauli ya baba askofu.Anapenda kuamini kuwa askofu ametoa msimamo wake binafsi na siyo tamko la kanisa wala maoni hayo siyo mafundisho rasmi ya kanisa.Askofu anapinga mgomo wa madaktari kwani ni kinyume cha maadili,anawataka wawe na huruma na watumie mbinu mbadala kudai madai yao.

  Hata hivyo anakubali na kusema kuwa hawa ni watu muhimu sana.Sasa kwa nini nampinga askofu.Kwanza askofu hakuweka lawama zake sawasawa kwa upande wa serikali badala yake amewaangalia tu madaktari,pili askofu anajaribu kujenga picha kuwa madaktari ndiyo wanasababisha wagonjwa kukosa huduma kwa kugoma kwao badala ya serikali ambayo imekataa kutimiza madai ya madaktari.

  Fundisho la kanisa linaruhusu migomo kama hatua muhimu na wakati mwingine ya lazima kwenye kudai haki za raia.Kanisa linataka serikali iimarishe na kuboresha huduma za jamii ili wale wanaofanya kazi wafurahie matunda ya kazi zao na wajisikie kufanya kazi zaidi,pia serikali inapaswa kuhakikisha uwepo wa haki za binadamu.Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasema kuwa mshahara wa haki(siyo mkubwa) ni matunda halali ya kazi.kukataa kulipa au kuzuia malipo ni grave injustice..

  Mishahara inapaswa kumwezesha mtu kuendesha maisha yenye staha kwake mwenyewe, watoto na familia yake.

  Migomo ni halali kimaadili(KKK) Pale inapokuwa haiwezi kuzuilika au ikiwa njia nyingine zimeshindikane au ikiwa ni lazima ili kupata faida fulani (proportionate benefit) .Sasa baba askofu anaweza pia kuulizwa maswali haya.je serikali imetoa mishahara ya haki kwa madaktari? na wanaendesha decent life?

  Je serikali imeimarisha huduma za jamii zikiwemo matibabu kiasi cha kuwafanya wafanyakazi kufurahia kufanya kazi zao? je, mgomo wa madktari umetokea kwa sababu madaktari wamependa au ni baada ya njia zote kushindikana kutokana na serikali kawadharau na kutowasikiliza?

  Kama majibu yote ni hapana ni vipi tena askofu asipinge ukosefu wa haki serikali inaofanya kwa watanzania hawa badala yake anakemea madaktari. na je mantiki inaonyeshaje kawa madakatari na siyo serikali ndo wanasababisha mateso ya watu,mimi nadhani lawama zote ziende kwa serikali,Tatizo kwa askofu kilaini anayeongoza serikali kwake ni chaguo la Mungu na hajawahi kusema kama Mungu alishajitenga naye.Labda anaona akikemea serikali atakuwa amefanya kufuru kwani atadharau mteule wa mungu.

  Vinginevyo Mgomo wa madaktari haujavunja maadili yoyote ya taifa, dini na hata udaktari wenyewe.Napingana na baba askofu na ninaunga mkono mgomo wa madaktari hadi serikali itakapotimiza madai yao au itakapojiuzuru.maswali kama watu wanakufa nk yanayo majibu ya kuridhisha(ANDISHI HILI NI MWITIKO KWA HABARI ILIYO KWENYE www.mjengwablog.com)
   
 2. k

  katitu JF-Expert Member

  #2
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  That is childish aguments think twice.Kilaini is a cleg man not a politician but you seem to be a politician something bad for a journalist like you.
   
 3. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #3
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Sasa unapinga nini??? furaha yako ni kuona watu wanakufa pale muhimbili, kisha wewe kushangilia kuwa unaikomoa serikali, always dini haiko kwa mambo ya dunia hii kaka!! think before posting here!!
   
 4. Plato

  Plato JF-Expert Member

  #4
  Feb 9, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 421
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 33
  So for you Kilaini is infallible and or impeccable? what when he is failing to rebuke the government which is central to the cricis? ok remain where you are
   
 5. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #5
  Feb 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,776
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  KILAINI mbishi kweli kwanini asiwaambie wafuasi wake athari za ufisadi au haoni jinsi kanisa lake linavyoukumbatia ufisadi mpaka wanaalikana kuchangishana fedha.....

  Watu wanadai maslahi yao yeye anajifanya anauluma sana na hayo madili ya madrug yanayowaua wa tanzania kwanini asipige kelele......huyu anashindana na LUSSEKELO a.k.a MZEE WA UPAKO kusapply maujinga na HURUMA za kinafiki..

  Kama KILAINI huna cha kuongea BABA askofu ni vyema ukafunga DOMO kwani viongozi wa DINI mpo weeeeeeeengi..umepelekwa BUKOBA atleast upumzike kuropoka still na uko umeanza labda wakupeleke SOMALIA ndo utanyamaza.......akhaaaaakh!:lol:
   
Loading...