Mgombea wa CCM ahamia rushwa ya vitabu

Mgombea wa CCM ahamia rushwa ya vitabu

imbuli

Member
Joined
Oct 20, 2014
Posts
16
Reaction score
1
MGOMBEA CCM AHAMIA RUSHWA YA VITABU;

Kuelekea miezi ya uchaguzi mengi yameendelea kujitokeza na wenye kutamani kufika pale alipo JK wameendelea kutafuta mbinu mbalimbali za kuweza kushawishi wapiga kura wao.

Asubuhi napita kusalimia katika ofisi za Umoja wa Vijana ambako ndiko ninako wajibika ghafla nashangaa kuona Katibu wangu ananipokea na Kitabu chenye nasaba ya mmoja kati ya Vijana wanaogombea Uraisi Ndgu. JANUARY MAKAMBA chenye kichwa cha habari Maswali 40 ya Karugendo kwa January.....

Kwanza niliuliza kinauzwa bei gani nikaambiwa Mwenyekiti ni zawadi yako hiyo na imetolewa kwa viongozi wote wa Mkutano wa CCM wa Taifa.........

Sikushtuka sana manake akili ilinipeleka mbali kwamba sasa hii ni aina mpya ya rushwa ambayo MANGULA hatokaa aione. Hivi kweli leo unawapa wajumbe Kitabu chenye kurasa zaidi ya 200 ili iweje?? Kwanza muda wa kusoma uko wapi?? Na kwanza nasoma nini?? Halafu huyu muhusika uwezo wake wa kiuandishi ameugundua lini?? Alikuwa wapi siku zote?? Na ni kws nini afanye iwe dezo wa watu wa CCM tu tena wapiga kura ndani ya chama?? Hivi kama huu si upunguani ni nini

Yaani JANUARY kwa kweli umekuwa janga sasa. Umeanza staili mpya ya kuhonga Vitabu........ tatizo umesahau kuwa raha ya Kitabu ni mtu akitolee jasho kwa kukinunua ili awe na uchungu wa kukisoma braza lakini hii ya kuhonga kwanza mi nimekichoma manake ni kama vile unanipotezea muda wa kwenda kuweka sawa kura za Mteule wa Mungu yule yule ambaye amekuwa jiwe kuu la pembeni, yule yule aliyetoka ili kulinda heshima ya Nchi, yule yule mwenye uwezo wa kiungu.....

Like seriously hivi Makamba wewe leo wenzio wanaumwa, wanatafuta ada wewe unapeleka Pamphlets zako....... Nawe wajifanya Dream from my father.........

Rudi Jimboni kapange madiwani wako usije ukakosa yote walisema wakubwa "Mtaka Yote Kwa Pupa Hukosa Yote....."
 
Back
Top Bottom