DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
(CCM), Samia Suluhu Hassan ameahidi kutekeleza miradi mikubwa ya miundombinu, afya na kilimo mkoani Morogoro endapo ataendelea kupewa ridhaa ya kuwaongoza Watanzania baada ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29, 2025.
Akizungumza leo, Ijumaa Agosti 29, 2025, katika kampeni mkoani humo, Samia amesema Serikali itajenga barabara ya Bigwa–Mvua–Kisaki na kukamilisha ujenzi wa barabara ya Ubena–Zomozi–Ngerengere ndani ya miaka mitano ijayo.
Aidha, ameahidi kuimarisha huduma za afya wilayani humo kwa kujenga vituo vipya viwili vya afya, zahanati saba, pamoja na kukamilisha ujenzi wa zahanati nne unaoendelea hivi sasa. Sambamba na hilo, aliwahimiza wananchi kujiunga na bima ya afya ili kujihakikishia huduma bora za matibabu.
“Tunataka watu wote wa Ngerengere tuwe na bima ya afya. Msimu uliopita, mazao tuliyouza yameleta zaidi ya shilingi bilioni 11 mikononi mwa wakulima, na wafugaji nao wameingiza kipato. Ni jambo la busara kutumia sehemu ya fedha hizo kununua bima ya afya kwa familia zenu ili muendelee kupata matibabu mwaka mzima,” amesema Samia.