Mgombea ubunge Siha afarijika kuona bendera ya CHADEMA

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,795
Reaction score
5,255
Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel amefarijika kuona bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake wa Makiwalu wakati akifanya kampeni za kugombea Ubunge wa jimbo.

"Niwaambie makamanda bado nina wapenda na kuwaheshimu ndiyo maana nimefarijika kuona bendera hizi mbili (CHADEMA) na (CCM) zipo hapa lakini mmeniwekea kwa namna nzuri kwamba mmeiweka ile juu na mmeonyesha dalili kwamba tutaishusha hii ya chini tuendelee kujenga Siha, mimi leo ni limao nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo na watu wapate maendeleo" alisema Mollel Mbali na hilo Dkt. Mollel amedai kuwa anakumbuka mchango wa makanda hao ambao waliweza kusimama na yeye na kulinda kura mpaka siku alipotangazwa kuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia CHADEMA.

Chanzo: IPP Media
 
"Nilidhani vichaa wameisha duniani kumbe bado wapo".. MWALIMU NYERERE..
 
Majuto ni mjukuu, kumbe doctor huko aliko sasa hana amani kabisa, dhambi ya usaliti inamtafuna.
 
A
Mgombea Ubunge wa jimbo la Siha kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Godwin Mollel amefarijika kuona bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye mkutano wake wa Makiwalu wakati akifanya kampeni za kugombea Ubunge wa jimbo.

"Niwaambie makamanda bado nina wapenda na kuwaheshimu ndiyo maana nimefarijika kuona bendera hizi mbili (CHADEMA) na (CCM) zipo hapa lakini mmeniwekea kwa namna nzuri kwamba mmeiweka ile juu na mmeonyesha dalili kwamba tutaishusha hii ya chini tuendelee kujenga Siha, mimi leo ni limao nimekuja kuondoa kichefu chefu cha maendeleo na watu wapate maendeleo" alisema Mollel Mbali na hilo Dkt. Mollel amedai kuwa anakumbuka mchango wa makanda hao ambao waliweza kusimama na yeye na kulinda kura mpaka siku alipotangazwa kuwa Mbunge wa jimbo la Siha kupitia CHADEMA.

Chanzo: IPP Media
Alichokifanya Daktari Mollel kitamsumbua sana hadi siku anaingia kaburini
 
Wananchi wenzangu wa Siha toeni adhabu kali kwa huyu Mollel msimpe kura tena kwani aliwaacha na njaa akakimbilia kwenye shibe hawapendi huyu mtu kabisa nankama angewapenda angewatete ila nawaamini watu wa Kaskazini sana sio wa kudanganyika hasa wa Siha pigeni chini huyu kibaraka chukueni elfu 7 zao piteni hivi .
 
Back
Top Bottom