Mimi nimependa Xuma alivyotumia neno Ndugu katika mada yake! Ni rahisi sana kukimbilia matitle makubwa makubwa kama Bwana, Mheshimiwa nk.
Ninakubali pia kuwa ni muhimu kufichua uovu katika jamii, lakini ni nani na kwa ajili gani sasa yananitia mashaka. Ndg Godbless wa Arusha sio mara yake ya kwanza kuonekana mbele ya jamii na kama kuna madudu aliyoyafanya miaka nenda yangekuwa yamejulikana. Sawa na Ndg Mukasa(Oscar) ambaye baada ya kuona anaelemewa na mpinzani wake anamsukia kashfa, nako Arusha wapinzani wa Ndg Gobless watakuwa wanazidiwa sasa wanatafuta kumchafua; kama vile ilivyokuwa kwa Ndg yetu Slaa.
Tuchukue tahadhari, wengine ni wachafuzi tu, sio waibuaji wa maovu yaliyo ndani ya jamii yetu