Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi

Mwakaboko King

JF-Expert Member
Apr 22, 2015
1,099
207
Kama ulikua haujui ni wakati wako sasa wa kuendelea kujifunza kuhusu masuala ya chaguzi mbalimbali za Tanzania. Nchi yetu inatumia Mfumo wa Uchaguzi ambao Mgombea anayepata Kura nyingi halali kuliko Mgombea mwingine yeyote ndiye hutangazwa kuwa mshindi (First – Past – the Post).

Hii, ni kwa mujibu wa Ibara ya 41(6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, Kifungu cha 35 F(8) na 81(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Kifungu cha 82(a) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292.

Katika hili hakuna miujiza, kama wewe ni mgombea wa nafasi yoyote wingi wa kura zako halali kuliko wagombea wengine unaochuana nao utakupa ridhaa ya kutangazwa na Tume kuwa mshindi. Pia ni vema tukakumbuka kuwa Chaguzi za Tanzania zinasimamiwa na kuratibiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuzingatia; -

  1. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977)
  2. Sheria ya Taifa ya Uchaguzi (Na. 1 ya 1985) Sura ya 343
  3. Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa (Na. 4 ya 1979) Sura ya 292
  4. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Wilaya (Na. 7 ya 1982) Sura ya 287
  5. Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka za Miji ( Na. 8 ya 1982) Sura ya 288
  6. Sheria ya gharama za Uchaguzi
  7. Sheria ya Uraia Na 6 ya 1995
Nawatakia siku njema.
 
Back
Top Bottom