Mgogoro wa Mgiriki Sotiris na Tajiri Mushi ulikwisha?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,307
4,585
Nakumbuka mwaka 2013, tajiri Willken Mushi wa Arusha, alituma zaidi ya vijana 20 kwenda kuvunja nyumba tatu alizokuwa akiishi mgiriki Sotiris Sotirindes ambaye kipindi hicho alikuwa ana miaka 87. Mushi alikuwa akidai kwamba aliuziwa eneo hilo na chama cha kahawa Arusha, ingawa hakuwa na hati za kuthibitisha umiliki.
Huyu mzee Sotiris yupo au alijifia? Na huyo Mushi bado anadunda?

POSTED SUNDAY, FEBRUARY 24, 2013 | BY- PETER SARAMBA, ARUSHA
DC aamuru maofisa ARCU wakamatwe
MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munasa, juzi aliamuru kukamatwa na kusekwa rumande, watendaji

MKUU wa Wilaya ya Arumeru, Nyirembe Munasa, juzi aliamuru kukamatwa na kusekwa rumande, watendaji wawili wa Chama Kikuu cha Ushirika cha Mkoa wa Arusha (ARCU) na walinzi wanne wa Kampuni ya Ulinzi ya Foday, kutokana na tukio la nyumba tatu za kikongwe Sotir Sotridad (87), kuvunjwa kinyume cha sheria.

Munassa anayekaimu ukuu wa Mkoa wa Arusha, alimwagiza Ofisa Ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Jeremia Goroba, kuanza taratibu za kufuta hati miliki ya shamba la ARCU lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 200, ili ligawanywe kwa wananchi wenye shida ya ardhi kulingana na utaratibu wa mipango miji.

Alifikia hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Kijiji cha USA-River, Kitongoji cha Chemichemi na kushuhudia mzee huyo na familia yake, akilala nje baada ya waliomvunjia nyumba kuchanachana mahema aliyopewa na Rotary Club ya Arusha.

“Huu ni unyama usiovumilika. Eti kwa sababu ana fedha, mtu anavunja nyumba ya mzee kama huyu bila nyaraka au amri yoyote halali ya mahakama kana kwamba hakuna Serikali inayoweza kulinda na kutetea haki za raia wake,” alisema mkuu huyo wa wilaya.

Maofisa wa ARCU ambayo kulingana na nyaraka ndiyo wamiliki halali wa eneo la zaidi ya ekari 200 ikiwemo eneo lenye mgogoro, Looti Long’odu na Clavery Mkwawa walijikuta matatani baada ya kushindwa kueleza sababu zao kama wamiliki halali, kumruhusu mtu mmoja kuvunja nyumba ya bibi huyo kinyume cha sheria.

Walinzi wa Foday Security wanaolinda eneo hilo kumzuia Mzee Sotridad kufanya ukarabati wala kujenga mahema kujihifadhi ambao majina yao hayakuweza kujulikana mara moja waliponzwa na ujeuri wa kukataa kufika mbele ya mkuu wa wilaya walipoitwa wakidai kuwa hawawajibiki kwa kiongozi huyo wa Serikali bila uongozi wa kampuni yao.

Nyumba za kikongwe huyo zilivunjwa Februari 8, mwaka huu baada ya watu zaidi ya 20 waliokodishwa na mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha kumfurusha nje kikongwe huyo aliyelazimika kusimama akishuhudia mali, nyaraka na vitu mbalimbali vikichukuliwa na wavamizi.

DC aamuru maofisa ARCU wakamatwe


DC Arumeru amwamuru Mushi amjengee Sotirides nyumba ndani ya wiki moja!
10/2/2013

MKUU wilaya ya Arumeru Nyirembe Munasa amemwamuru mfanyabiashara maarufu jijini Arusha, Willken Mushi aliyevamia eneo linalomilikiwa na raia wa Ugiriki, Sotiris Sotirindes (87 ) na kufanya uharibifu mkubwa ikiwemo kuvunja nyumba aliyokuwa akiishi, kumjengea nyumba nyingine haraka kwa muda wa wiki moja, sanjari na kumpiga marufuku kukfanya shughuli nyingine zozote katika eneo hilo.
Nakuagiza kuanzia sasa ufike katika nyumba hiyo na ukamwombe msamaha raia huyo, na kisha umjengee nyumba ya kuishi kwa sasa hivi kutokana na kuwa anaishi na kulala nje tangu Jumatatu ulipombomolea nyumba yake, na pia huna ruhusa yoyote ya kuendelea kufanya shughuli zozote katika eneo hilo hadi hapo utakapoleta vithibitisho vya umiliki wako katika eneo hilo.
388207658.JPG


Nyerembe alitoa kauli hiyo ofisini kwake wilayani Arumeru katika kikao kati yake, Mfanyabiashara, Afisa Ardhi wa wilaya ya Arumeru pamoja na Familia iliyokubwa na adha ya kuvunjiwa nyumba yao iliyokuwepo katika kata ya Usa River kitongoji cha Chemichemi wilayani humo.

Alisema kuwa, hatua ya Mgiriki huyo kuingiliwa shambani kwake na kuharibiwa mazao yake ikiwemo kuvunjiwa nyumba anayoishi huku akiwa ndani, ni ukiukwaji mkubwa sana wa sheria, kwani sheria hairuhusu mtu yeyote kuvamia nyumba ya mtu bila kuwa na taarifa ya kimaandishi.


Mkuu huyo alionyesha wazi kukerwa na hatua ya baadhi ya wafanyabishara kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia fedha zao , kuwanyanyasa watu wenye kipato kidogo bila kujali kwamba suala hilo lipo ngazi wa mahakama.

Mkuu wa Wilaya alipomtaka Mfanyabiashara huyo kuonesha vielelezo vya kumiliki eneo hilo (building permit), alisema hana. Alipotakiwa kuonesha barua inayoonyesha makabidhiano ya eneo hilo kati yake na ACU pia hakuwa nayo. Badala yake, Mfanyabiashara huyo alieleza mbele ya mkuu wa Wilaya kuwa aliuziwa eneo hilo na ACU tangu mwaka 2002 hivyo eneo hilo ni mali yake halali.

Alipoulizwa, Afisa Ardhi wa wilaya ya Arumeru, Jeremia Wilson yeye alikana kupokea maombi yoyote yaliyowasilishwa na Mfanyabiashara huyo kuhusiana na eneo hilo ama barua yoyote inayohusu uhamisho wa umiliki wa eneo hilo. Afisa Ardhi akasema hadi sasa, kumbukumbu zinaonesha wazi kuwa, mmiliki wa eneo hilo ni Mamlaka ya Kahawa (ACU) ingawaje Sotiris anamiliki eneo hilo tangu mwaka 1978 (zaidi ya miaka 34) akiwa na mgogoro na ACU ambapo shauri lao lipo katika ngazi ya Mahakama ya Ardhi ya Mkoa.

Munasa akasema kuwa, kwa mujibu wa sheria za ardhi mtu akishakaa kwenye ardhi kwa zaidi ya miaka 12 anastahili kulimikishwa eneo hilo, na hapa raia huyo anadai kukaa katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30.
479922254.JPG


Kwa upande wake, Sotiriades alimweleza mkuu huyo kusikitishwa na kitendo cha kinyama alichovamiwa na watu zaidi ya 20 katika nyumba yake na kuharibu baadhi ya vitu vyake ikiwemo uporaji wa vitu mbalimbali huku akiamriwa kuondoka katika eneo hilo huku akitukanwa kwa matusi makubwa na kutupiwa maneno ya kejeli.

Alisema kitendo hicho kimemfedhehesha sana kwani yeye sasa ni mzee hajiwezi na anahitaji msaada wa kibinadamu. Akasema baada ya kuvunjiwa nyumba hiyo tangu Jumatatu amekuwa analala nje akipigwa baridi kali usiku bila msaada wowote.
Mimi nimekuwa nikiishi katika eneo hilo kwa zaidi ya miaka 34 hivi sasa na sijawahi kupata shida yoyote ile, ila nimeshangaa sana kukumbwa na hali kama hii bila taarifa yoyote. Sijawahi kulala nje na wala sikutegemea hivyo katika maisha yangu.
Alimwambia Mkuu huyo kuwa, Mushi alikuwa alimtolea maneneo ya kejeli kwa kumwambia ni lazima aondoke kwenye nyumba hiyo amfuate mama yake alipo huku akisisitiza kuwa hata akimfuata mkuu wa mkoa, Rais Kikwete, Mkuu wa Wilaya, RPC, Kwa hakimu yeyotem hatambabaisha kwani yeye anazo pesa.

Hata hivyo alishukuru Serikali kwa kuingilia kati mgogoro huo huku akisema kwamba hali hiyo inaweza kusaidia kwa watu wanaoonewa na wenye kipato kikubwa kupata haki zao za msingi zilizodhulumiwa.

Naye Naftari Komba, mama anayeishi na Soritiades alisema anashangazwa sana na hatua ya mfanyabiashara huyo kuvamiwa nyumba yao na kuharibu shamba lenye zaidi ya hekari 7 ambalo walikuwa wamelima mazao mbalimbali ya chakula na kuharibu mazao yote kwa kutumia trekta.

Aliongeza kuwa, kitendo cha mfanyabiashara huyo kuvamia shamba hilo kumeonyesha wazi kuwa ni jinsi gani watu nwenye fedha wanavyoweza kudharau mahakama na kutotii amri ya mahakama kwani kesi kuhusu eneo hilo bado ipo katika Mahakama ya Ardhi na kuwa angesubiri kesi iishe ndipo ajue hatua ya kuchukua.
Source: Wavuti
 
Back
Top Bottom