Mgogoro wa Marekani na Korea ya Kaskazini una madhara gani kwetu?.

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Jan 26, 2012
540
507
Mgogoro wa Marekani na Korea ya Kaskazini una madhara gani kwetu?.

Kwanza tunatakiwa tutambue kuwa huu mgogoro ni mbaya si kwa nchi hizi mbili tu, yaani Marekani na Korea ya Kaskazini. Ni kuomba sana waishie kwenye vita hii ya maneno na si vitendo. Mgogoro huu uko kiuchumi zaidi, kwa sababu kiuhalisia kabisa kama unataka uzidi kuwa Taifa kubwa, unatakiwa uwe imara zaidi kuliko wenzako kiuchumi na Kijeshi. Ukiwa imara maeneo hayo mawili Duniani, wewe ni Taifa kubwa zaidi Duniani yaani (Super Power). Ndiyo maana Marekani ni Super Power kwa miaka mingi sasa. Wako imara zaidi kiuchumi na kijeshi kuliko Taifa lolote lile. Na huwa hawafurahishwi sana na yoyote atakayekuwa anakuja taratibu katika hatua hizo mbili. Naweza kusema kwamba, mgogoro huu, ukiacha na Korea ya Kaskazini kujihusha na maswala ambayo wanasema wao (Marekani) yanakiuka makubaliano ya Kidunia ya kuzalisha siraha hatari kabisa hasa za nyuklia. Na sababu ya pili ni hii ya uzalishashi wa siraha za nyuklia. Swali ni Je, Mareakani na wengine hawana siraha za nyuklia??. Kama ni Korea ya Kaskazini tu ndiyo mwenye siraha hizi basi ni hatari zaidi na zaidi. Lakini wadadisi wa maswala ya mambo ya Vita na Matumizi ya siraha wanajau na hata ukigoogle utapata ukweli.

Endapo Marekani na Korea ya Kaskazini wataendelea na taharuki hii iliyopo kwa sasa, huko mbele mambo yanaweza kuwa mabaya zaidi si huko kwao bali na kwetu Afrika. Kiuchumi,misaada ambayo tunaipata kutoka Marekani na hata nchi za Ulaya na Mashariki hasa Uchina kuna hatari sana zikakoma endapo kutatokea vita. Kwa hiyo, ni swala la kutoombea kabisa vita hii isitokee.

Pia, kwa nje tunaona vita ni ya wawili, lakini kama mnajua kwamba kuna nchi za Magharibi yaani kila kilanja Mkuu ni Marekani. Hawa ni NATO, na yoyote mwenzao akiwa vitani lazima wamsaidie kwa udi na uvumba kwa uwazi au kwa siri kubwa. Pia, kuna nchi ambazo ziko Ukanda wa Mashariki kilanja wao Mkuu ni Urusi, ambayo ni nchi ya pili kwa ubora kijeshi Duniani. Hawa nao mmoja akivamiwa wengine mara nyingi hyingilia kati kumsaidia.

Na makundi haya ya uhasama kati ya USA na Korea ya Kaskazini kama yalivyo Urusi na Marekani yalitokea baada ya vita ya kwanza ya Dunia (WW01 June 28,1914-Nov 11, 1918). Na yakaja kukolezwa na vita ya pili ya Dunia (WW02 Sep 11, 1939-Sep 02,1945). Kuna vita vilivyofuata baadae ambavyo vilikoleza uhasama kati ya makundi ya Mashariki (Urusi na wafuasi wake) na Magharibi (Marekani na wafuasi wake). Kwa mfano, vita vya Vietnam 1955-1975. Pia, vita ya Korea ya 1959-1953 ambayo ilipelekea Korea kusambaratika na kuwa Korea ya Kusini na Kaskazini. Na moja ikiwa upande wa Magharibi yaani Korea ya Kusini na nyingine ikiwa upande wa Mashariki yaani Korea ya Kaskazini. Vita baridi vya 1985 mpaka 1991 ndizo zilizidisha uadui zaidi kati ya Marekani na Urusi. Na hapo miaka ya 1989 Muungano ya Kisoshalist yaani (the Societ Union and it's Satellite States ulivunjika.

Katika mgogoro huu kwa sababu ya Historia ilivyo kama nilivyoielezea kuna nchi baadhi kutoka Mashariki kulingana na Historia ziko upande wa Marekani kama Korea ya Kusini, Japani na baadhi ya nchi. Na kuna nchi ziko Korea ya Kaskazini kwa kisiri au uwazi kama Urusi, China, Irani na nchi zingine za Mashariki mwankati. Kwa hiyo, ikitokea vita kusema kweli hata sisi Afrika hatuko salama kiuchumi na kisiasa kwa sababu ya mulengo yetu ilivyo na kwa utegemezi wetu.

Suluhisho kubwa ni kuanza kuhubiri kama wakina Nyerere walivyokuwa katika vita baridi ya kutofungamana na upande wowote ule. Japo hii njia ilitumika vizuri sana maana kuna muungano mkubwa ambao ulijijengea sifa kubwa kwamba hata vita ikitokea wao hawako upande wowote. Je, bado hali hii ipo??. Maana Muungano huu kama ulishakufa kabisa kwa sababu nchi nyingi ambazo zilikuwa humu wakati huo kiuchumi hazikuwa sawa kabisa.

Tuombe mambo haya yasitokee na yawe ni ya mdomo tu. Itategemea na Emotional Intelligence ya Trump zaidi katika hili.

Na hili likitokea tusidhani litabaki la uadui wa mitandaoni kama ambayo huwa tunashangilia kama tunavyodhani; tusifikiri ni vita kama ile ya Team Diamond na Kiba. Hii si vita kama ya Team Wema na Zari. Hapa ikitokea na ikasambaa ni vita ya kuonyesha ubora wa siraha kali na za maangamizi zaidi. Watakaoasirika ni watoto, wakina Mama na Vijana wengi. Na mataifa mengi yatakuwa na taharuki kubwa sana.

Tumwombe Mwenyezi Mungu aepushie mbali.

18/04/2017
 
kwahyo ulusi ni ya piri kwa kuwa na nguvu duniani kijeshi?malekani na kolea pia wako vizuli kuriko nchi yoyot
 
Back
Top Bottom