Mgogoro ndani ya NATO

Mgogoro ndani ya NATO

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,599
Katibu Mkuu wa NATO akiri kushtadi mzozo ndani ya shirika hilo la kijeshi

Nchi wanachama wa Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO), zimershiriki katika kikao cha maadhimisho ya mwaka wa 70 tangu kuasisiwa taasisi hiyo ya kijeshi katika hali ambayo tofauti na changamoto kubwa ambazo hazijawahi kushuhudiwa huko nyuma, zinauweka mustakbali wake katika hali isiyojulikana.

Tofauti juu ya sababu ya kuundwa na umuhimu wa NATO, ndio chanzo kikuu cha tofauti za hivi karibuni za muungano huo wa kijeshi. Suala hilo limewapa changamoto kubwa viongozi wa shirika hilo, hususan Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wake.

Katika uwanja huo, Jumatatu iliyopita, Stoltenberg alinukuliwa akisema kuwa, Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO linakabiliwa na anga mbaya zaidi ya kiusalama na wimbi la mizozo kati ya nchi wanachama, tangu taasisi hiyo iundwe.

Matamshi hayo yametolewa katika hali ambayo kikao cha hivi karibuni cha viongozi wanachama wa NATO mjini London Uingereza, kilishuhudia tofauti kali hususan kati ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na Rais Donald Trump wa Marekani.

Jens Stoltenberg ambaye alikuwa akizungumza nchini Kuwait kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 15 wa mpango wa 'Ubunifu wa Ushirikiano wa Istanbul' (ICI) alisema: "Tulikuwa na maadhimisho ya mwaka wa 70 wa Muungano wa Kijeshi wa NATO mjini London na kwa miaka yote hii tulikuwa hatujawahi kushuhudia NATO ikikumbwa na anga ngumu ya kiusalama kama iliopo kwa sasa.

"Kuibuka tofauti ambazo hazijawahi kushuhudiwa kati ya Ufaransa, Marekani na Uturuki kunatokana na misuguano ya wanachama hao wa NATO katika uga wa masuala ya kiulinzi na kijeshi ambapo moja wapo ya tofauti hizo ni hatua ya Washington ya kuipa kibali serikali ya Uturuki kufanya mashambulizi kaskazini mwa Syria bila ya kujiri maushauriano wala kuwepo ushirikiano na wanachama wengine wa shirika hilo la kijeshi.

Suala hilo lilizua malalamiko makali ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ambaye alitoa matamshi makali kwamba muungano huo umekumbwa na kifo cha ubongo.

Hata hivyo matamshi hayo ya rais wa Ufaransa mbali na kwamba yalikuwa yanalalamikia hatua ya Uturuki na Marekani, yalikabiliwa na radiamali kali ya Ujerumani ambayo nayo ni mwanachama muhimu wa Ulaya ndani ya NATO na pia kutoka kwa Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa muungano huo.

Katika uwanja huo tarehe 16 ya mwezi huu na katika kikao mjini Istanbul Uturuki, Stoltenberg kwa mara nyingine sambamba na kukosoa matamshi hayo ya rais wa Ufaransa, alisisitiza kwamba NATO inaweza kuondoa tofauti zake na kufikia uwezo mkubwa wa ustawi.

Aidha Ujerumani ilijibu matamshi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kwa kusisitizia umuhimu wa kudumishwa maendeleo na udharura wa shirika hilo kuilinda Ulaya. Katika uwanja huo Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel alisisitiza kwa kusema: "Muungano wa kijeshi ambao umekosolewa na Rais Emmanuel Macron, unatakiwa ulindwe daima.

Kulindwa NATO ni kwa maslahi yetu hata kuliko kipindi cha vita baridi." Kwa utaratibu huo si tu kwamba tofauti kuhusiana na falsafa ya kuwepo na umuhimu wa muungano huo zipo kati ya wanachama wa Ulaya na wasio wa Ulaya, bali mpasuko katika uwanja huo kati ya wanachama wa Ulaya yaani Ujerumani na Ufaransa zimeongezeka zaidi.

Licha ya radiamali hizo dhidi ya rais wa Ufaransa, lakini ukweli bado upo wazi, nao ni mgogoro kuhusu nafasi na jukumu kuu la uwepo wa NATO ambao hapo awali kwa akali ulikuwa ukitekeleza hatua za kiusalama kwa msingi wa mashauriano na ushirikiano wa wanachama wake.

Kuhusiana na suala hilo Anders Fogh Rasmussen, Katibu Mkuu wa zamani wa NATO ambaye alianza kushikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 2009 hadi 2014, sambamba na kuthibitisha juu ya uwepo wa tofauti kubwa kati ya wanachama wa muungano huo wa kijeshi, alisema kuwa tofauti hizo hazijawahi kushuhudiwa katika historia yake.

Sababu nyingine muhimu ya kushtadi tofauti ndani ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO ni juhudi za wazi za nchi za Ulaya kwa ajili ya kuanzisha mfumo tendaji wa kiulinzi wenye kujitegemea wa Ulaya unaoongozwa na Ufaransa. Hii ni kwa kuwa Trump hajafurahishwa na mwenendo wa serikali ya Paris kuanzisha na kuimarisha asasi na miundo ya kujitegemea kiulinzi kwa ajili ya Ulaya, ambapo kwa mara kadhaa amekosoa pia hatua hizo.

Wakati huo huo hatua za hivi karibuni za Marekani na Uturuki za kufanya mashambulizi kaskazini mwa Syria na bila ya kuwashauri wanachama wengine wa NATO, zilibainisha kuwa muungano huo taratibu unapoteza majukumu yake makuu yaani ya kuimarisha mashauriano kati ya wanachama wake kuhusu masuala muhimu ya kiulinzi na kijeshi.

Ukweli ni kwamba ni muda sasa ambapo Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi NATO umekuwa na mpasuko na mgogoro mkubwa wa ndani kuhusu lengo la kuundwa kwake, ingawa baadhi ya wanachama wa muungano huo hawataki kukiri ukweli huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom