MGAWANYO WA KEKI YA TAIFA.
Wananchi wa Mtwara wame​andamana kukataa gas ku​safirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar. Wananchi wa Mtwara wamejifunza mengi kutokana na faida ya rasilimari za nchi hasa mgawanyo wa rasilimali usio sahihi wala vipaumbele. mfano baada ya uhuru mikoa ya pembezoni mwa nchi imebaki nyuma kimaendeleo kwa kukosa huduma za umeme na barabara nzuri za rami kama mikoa mingine ili hali mikoa hiyo ikichangia katika pato la taifa kama mikoa mingine. Mikoa ya Rukwa, Kigoma, Mtwara na Lindi imebaki maskini kupita kiasi huku ikisahaulika katika mipango ya nchi. Miaka 50 baada ya uhuru ndiyo kidogo inaanza kupata barabara za rami huku mikoa mingine ikibadirisha rami zilizo choka zaidi ya mara 5, Ni miaka ya hivi karibuni tu baada ya mtwara kugunduliwa kwa gas ya mnazi bay ndiyo wamepata umeme wa uhakika la sivyo wangeendelea kuusikia tu. Pia wamshukuru Rais Mkapa kujitoa mhanga kwa kujenga barabara kuelekea huko. Na huu ndiyo mtindo wa viongozi wa sasa kujali maeneo wanayotoka kwanza. Mkapa alifanya hivyo kusaidia mikoa ya kusini anatoka japo alifanya vyema kwani hakuna aliyewahi kuliona hilo kama tatizo, pia Rais Kikwete nae anataka kufanya yale yale ya mkapa kwa kujenga bandari ya Mbegani huko bagamoyo, mpango kuifumua barabara ya segera chalinze na nk.
Kuna umuhimu gani wa kuibomoa na kuijenga upya barabara ya Chalinze Segera? Je, ni sahihi kujenga bandari nyingine Mbegani, wilayani Bagamoyo anakotoka Rais wa Jamhuri, Jakaya Kikwete, huku miundo mbinu ikiwa mibovu au kutofanya kazi kabisa? Je mipango hii ilikuwapo katika mipango mkakati wa nchi?
Kama reli haifanyi kazi kwa ufanisi, mizigo itakayoshushwa mbegani. kwenda bara na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Kongo na Zambia, itapitia wapi?
Tunasikia bandari ya Dar es salaam kuzidiwa kwa nini bandari za Tanga na Mtwara zisiboreshwe ili kupunguza huu msongamano? Wananchi wa mtwara wanataka viwanda vijengwe kwao ili na wao wapate ajira. Serikali isipuuze mawazo yao kwaani yanayotokea Nigeria kwenye ule ukanda wa mafuta yanaweza kutokea hapa kwetu pia hapo baadae. Tukiacha siasa Ushirikishwaji wa wananchi katika kuanzisha miradi mbalimbali ni muhimu sana hata prof Muhongo anajua.