Hili nalo ni Tatizo la Viongozi wetu na linatushangaza sana,kwajiji kubwa kama DSM kukosa umeme kuna athiri mambo mengi sana ya maendeleo kama mahopstali mabenki majumbani mwetu na sehemu nyingine nyingi,Mawaziri wengi wa Nishati na Madini wamepita lakini swala hili limekuwa kama Mradi kwao je ni kweli kuwa nchi yetu imekosa kabisa njia au nishati mbadala ya kulimaliza tatizo hili la mgao wa umeme ? au tuna kuwa na Mawaziri husika hewa?wakati kwenye kampeni tuliahidi mambo makubwa makubwa ya ajabu mfano,kujenga viwanja vya ndege kwenye Mikoa kadhaa,kununua Meli, kujenga Mabarabara,na hata za juu angani,kununua Bajaji 400 songea n.k