Sasa hivi imekuwa tabia ya mashirika yetu kutokutoa huduma bila taarifa. Tanesco baada ya uchaguzi kumalizika kuna mgao wa rejareja unaendelea. Kila siku umeme unakatwa tena kwa masaa mpaka 8 hakuna taaarifa ya maana. Jana Ngereja baada ya kuapishwa alisema wanataka kumaliza mambo ya mgao wakati tuko kwenye mgao wa kimyakimya. Hii kitu inachosha na kukera sana. Tutakuza uchumi kweli? Kwanini wasitangaze tu?