Ni mbilingembilinge la kufa mtu, Lori kubwa la manispaa ya Ilala likiwa sambama na gari dogo aina ya Land Cruiser sambamba na Mgambo wa kazi waliofura ipasavyo, wanaendelea kukamata biashara za wamachinga zilizozagaa mitaa ya posta mda huu,
Tayari wameshakamata bidhaa nyingi sana, na kila likijaa gari wanapeleka kwenye stoo yao iliyopo maeneo ya Kamata!