Mfungwa anapofariki kabla ya kifungo nini hufanyika?

prince uweri

Senior Member
Feb 6, 2016
112
88
Ndugu nisaidieni kidogo nini hutokea pale mfungwa anapofariki akiwa bado anatumikia kufungo chake. Je ndugu zake hupewa taarifa pamoja na mwili au kuna taratibu gani?
 
Anawekewa Pingu kwenye kaburi lake badala ya msalaba, mpaka pale kifungo chake kitakapokwisha, ( Hivi ndivyo tulivyokuwa tukiulizana na kujibizana tukiwa shule ya msingi) nadhani swali lako linatokana na uelewa huu, ngoja tusubiri majibu toka kwa wazoefu wa huko magereza.
 
Magereza wana pingu ngapi za kufunga makaburi ya maiti ya wafungwa na je kuhusu usalama wa pingu zenyewe ukoje na labda pia uchakavu wake kutokana na kunyeshewa na mvua na kupigwa na jua zitakuwa na ubora?
 
Lile eneo ambalo msalaba huchomekwa, inawekwa pingu kubwa na itakaa pale kipindi chote kilichosalia cha kifungo, kikimalizika basi wahusika watatoa hiyo pingu na kuweka msalaba.
 
Kwani hakuna alowahi kuwa mfungwa, akafa (sorry, akimaliza kifungo na kupata uzoefu) na kurudi uraiani awaeleze wakuu? Mimi sijui!
 
Ninachojua mimi kwani nimesha shuhudia jamaa yangu mmoja alifiwa na ndugu yake alikuwa ni mfungwa walitaarifiwa na kwenda kuchukua mwili wa ndugu yao na kwenda kuuzika. Labda kama ndugu wasipopatikana ndio jeshi la magereza litauzika mwili.
 
Ndugu nisaidieni kidogo nini hutokea pale mfungwa anapofariki akiwa bado anatumikia kufungo chake. Je ndugu zake hupewa taarifa pamoja na mwili au kuna taratibu gani?

Atakuwaje mfungwa kabla ya kifungo? Hebu fafanua. Ninavyofahamu mimi maana ya mfungwa ni mtu aliyeko kifungoni.
 
Lile eneo ambalo msalaba huchomekwa, inawekwa pingu kubwa na itakaa pale kipindi chote kilichosalia cha kifungo, kikimalizika basi wahusika watatoa hiyo pingu na kuweka msalaba.
Wanaweka msalaba kwani hao wafu wote ambao hawajamaliza kigungo ni wakristo?
 
Back
Top Bottom