Mfumo wa vyama vya siasa Tanzania Uangaliwe Vizuri, tusubiri kuona matukio mabaya

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,662
12,402
Mfumo wa vyama vya siasa Tanzania nilazima uangaliwa ktk sura ya pili au tusubiri kuona matukio mabaya huko mbeleni, mimi nikiwa kama mtu ninaye fuatilia siasa za taifa hili sioni kama vyama vya siasa tulivyo navyo sasa vina majibu ya sahihi kwa watanzania hasa ktk kipindi hiki tunapita kama taifa.

Tusikubali kuwa na vyama vinachochea kuvunja umoja wetu ushirikiano na hata utaifa wetu, nijambo lakushangaza vipo vyama vya siasa vinafanya watu kuishi kama paka na panya while sisi sote ni watanzania sura moja na lugha moja. vyama vya siasa vinavyotengeneza kamati za ulinzi kuwapa silaha nakuacha kutumia vyombo vyetu vya usalama wetu ni hatari kubwa ktk taifa eltu au kama wanaitaji ulinzi kwa nini wasitumie mashirika ya ulinzi je kuna agenda gani kwa hivi vyama.

Taifa hili limetoka mbali sana na tusichezee Amani yetu aina ya machama uchwara ambavyo nia yao kubwa nikututenganisha, vipo vyama vya kikabila, vyama vya kidini, vyama vya kikanda na hata vyama vya kifamilia. Hili nijambo la hatari ktk usalama wetu na ikiwa watu watakaa kimya vyma hivi mwisho vitatupelekea kubaya.

tusiangalie leo tiangalie kesho ya watoto wetu na vizazi vijazo kwakufuta vyma vya aina nilio taja.
 
Back
Top Bottom