Naomba JamiiForums ifungue mjadala kuhusu namna Mfumo wa Kitaifa wa Ununuzi wa Umma kwa Njia ya Kielektroniki (NeST) unavyotumika. Swali ni hili: Je, kila mzabuni anayekidhi masharti ya zabuni ya wazi anapata nafasi sawa ya kushiriki, au baadhi ya maafisa wanaweza kuamua nani aione zabuni, nani aruhusiwe kuwasilisha zabuni na nani abaki nje?
Tumepata changamoto hii kwa baadhi ya Zabuni haswa hizi za Taasisi na Almashauri, unakuta ulikuwa unapata notification mapema na kuingia kwenye ushindani ila ghafla miezi na miezi unakuta haupo kwenye list na wenzako unaowajua wapo na mnafanya biashara ya aina moja. Kibaya zaidi unaweza kupata notification mara baada ya zabuni kupita muda wake.
Tunaomba mfuatilie viashiria hivi vya Rushwa ama upendeleo unaoweza kufanywa na maafisa ununuzi/wajaza taarifa kwenye mfumo, je kuna uwezekano kujua ni makampuni mangapi yalialikwa kwenye zabuni haswa hizi min tenders? Je, wahusika (PMU) na maafisa wanaweza kuzuia wazabuni wengine na kuwapa upendeleo wachache wanaowajua na kufifisha dhima nzima ya ushindani wa manunuzi.?
Mfumo unaweza kutengenezwa kumlazimisha afisa anayeweka taarifa za zabuni husika kuchagua wazabuni automatically kutokana na mahitaji na si afisa kufanya kwa matakwa yake na kuondoa wengine?
Je, kumbukumbu za NeST zinaweza kuonyesha nani alibadilisha orodha ya walioalikwa au vigezo vya ushiriki, lini alifanya hivyo na kwa idhini ya nani? Na mzabuni anayezuiwa kushiriki anawezaje kupata sababu kabla ya muda wa zabuni kuisha?