Mfumo wa Live Updates hapa JF umepotelea wapi?

mkolaj

JF-Expert Member
Mar 24, 2014
3,020
1,087
Siioni Jf ya zamani ambayo members walikuwa wana-update matokeo ya michezo mbalimbali.
Ni mfumo ambao ulikuwa unalifanya hili jukwaa la michezo kuwa jukwaa linalopendwa na kuvuta members wengi ukiondoa lile la SIASA.
Tulikuwa tunakutana wanamichezo wa timu zote, kupongezana, kuchambana, pia hata kupeana majina ya utani kama mashabiki wa SIMBA kuitwa MIKIA, Yanga kuitwa YEBOYEBO, na Azam kuitwa MAKONTENA.

Siku hizi hakuna tena kitu kama hicho, siwaoni tena akina niffah, Sibonike, cnjona, graffan, Deo Corleon, Akina mkuu Makoye Matale, bantu lady na wengine wengi.

Wanajukwaa wenzangu tuurudishe tena ule mfumo ulikuwa mzuri kuliko ilivyo hivi sasa.

Ahsanteni sana
 
Mkuu, hata mimi nashangaa sana. nimejaribu kutafuta uzi wa live update wa mechi ya Yanga leo siuoni.
 
Sisi ndio wa kuurudisha mkuu, tatizo watu wamegawana timu za Ulaya kama mazombi vile....
 
tangu tufungwe 7 kwa 0 na algeria, jukwaa limepooza sana hili watu wamekata tamaa
 
Ule uchaguzi ulitupoteza sana aisee
Hivi unadhani mkuu Deo Corleone ule ubora wa Jukwaa hili utarudi tena kweli!! Siku kama ya jana ulipopigwa mkono wa wana wa jangwani tungekukimbiza kweli kweli!!
Jukwaa la Sports saivi limekuwa ni miongoni mwa majukwaa yasiyopendwa na wanajf, jukwaa limepoteza mvuto kabisa
 
Siioni Jf ya zamani ambayo members walikuwa wana-update matokeo ya michezo mbalimbali.
Ni mfumo ambao ulikuwa unalifanya hili jukwaa la michezo kuwa jukwaa linalopendwa na kuvuta members wengi ukiondoa lile la SIASA.
Tulikuwa tunakutana wanamichezo wa timu zote, kupongezana, kuchambana, pia hata kupeana majina ya utani kama mashabiki wa SIMBA kuitwa MIKIA, Yanga kuitwa YEBOYEBO, na Azam kuitwa MAKONTENA.

Siku hizi hakuna tena kitu kama hicho, siwaoni tena akina niffah, Sibonike, cnjona, graffan, Deo Corleon, Akina mkuu Makoye Matale, bantu lady na wengine wengi.

Wanajukwaa wenzangu tuurudishe tena ule mfumo ulikuwa mzuri kuliko ilivyo hivi sasa.

Ahsanteni sana

sheikh ondoa shaka, ada ya mtoto nimeshalipa na sasa sina deni, so now ni kujimwaga JF tu.
 
Jina la Makontena kwa Azam limeanza lini?
Jino hilo lilianza baada ya kampuni yao kuhusishwa na ukwepaji wa kodi bandarini

Na nakumbuka mm ndiyo nlileta baada ya kuona limeshamiri sana midomoni mwa mashabiki.wa mpira
 
Back
Top Bottom