Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,720
- 1,639
Habari wanajamvi,
Ni jambo la kufurahisha moyoni, kuwa ni mmoja ya wakufunzi wazuri wa Elimu katika eneo fulani, hakuna daina anayependa kuwa kiraza!
Tanganyika hapo mwanzo ilikuwa na mfumo wa Elimu wa kikoloni, mfumo ambao uliwawezesha wanafunzi kusoma hadi darasa la nne; (kama msingi) Kisha baada ya hapo walipaswa kuendelea kusoma hadi darasa la nane, huku mfumo wa ufundishaji Ukitanguliza mambo muhimu katika ulimwengu wa maisha ya kila siku katika kizazi hiki..
Mfumo huo wa Elimu haukuwepo hapa Tanzania Tu Bali ni kwenye nchi nyingi ambazo zilikuwa ni koloni la Uingereza.
Rais wa kwanza hayati Julias Kambarage Nyerere aliona mfumo huu wa elimu wa Waingereza ni mbovu, Hivyo mwishoni mwa miaka ya 70 Alibadili mfumo huo na kuanzisha mfumo wake.
Mbali na kwamba mataifa mengine mengi ambayo yalikuwa ni makoloni wa Uingereza yalikuwa na mfumo ule wa elimu ya kikoloni hayakuweza kuubadilisha kabisa, Mfano ndugu zetu Kenya.
Hili ni swali nilonalo kwenu wanajf? Je mfumo mpya wa Elimu wa Tanzania umeiinua Elimu yetu au Umeiua Elimu yetu? kama umeiinua umeiinua kwa asilimia ngapi ukifananisha na nchi za wenzetu (Koloni la Uingereza) na kama Elimu imekufa imekufa imekufa kwa kiasi Gani?
Na hatua gani ichukuliwe upesi kama Elimu yetu inazidi kudidimia?.
Nawasilisha...
Secret star.